28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Walalamikia Dawasa miundombinu yake kupoteza maji

Saidi Ibada Na Faustine Madilisha (TUDARCo)-Dar es Salaam

BAADHI ya wananchi wa Keko wameilalamikia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa), wakidai miundombinu yake imechoka hatua inayofanya mabomba kupasuka na wao kukosa huduma ya maji.

Diwani wa Kata ya Keko, Mohamedi Fundi, alisema viongozi wa kata hiyo hutoa taarifa mara kwa mara Dawasa kuhusu ubovu wa miundombinu ya maji, lakini utekelezaji umekuwa wa kusuasua.

“Sisi viongozi tunatoa taarifa kuhusu ubovu wa miundombinu katika eneo letu kwa kuwaandikia barua, tunawapigia simu, muda mwingine tunawafuata kuongea nao, lakini utekelezaji wao si wa kuridhisha,” alisema Fundi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Keko Mwanga, Shilingi Shilingi, alisema utengenezaji wa miundombinu bado ni changamoto kwani mafundi hutengeneza sehemu yenye tatizo pekee.

“Hatuwezi kuwalaumu  moja kwa moja kuwa hawafanyi kazi, lakini inatakiwa wafike mahali wakubali miundombinu yao si imara, wanaweza kutengeneza hapa, lakini hatua 15 mbele utakuta bomba limeharibika,” alieleza Shilingi.

Mhandisi  wa Dawasa, Wilaya ya Temeke, Ramadhani Sangai, aliwaomba wananchi kuwa na subira wakati mamlaka ikifanyia kazi changamoto hizo.

“Kila eneo lina timu yake, tuna ya Keko, Mbagala na Mfeni, hata hivyo mafundi wetu waliopo eneo la Keko Mwesi B wanaendelea na kazi, tunapokea taarifa nyingi  pengine hii haijatufikia wakati mwafaka,” alisema Sangai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles