Florence Sanawa, Mtwara
Serikali imesema maandiko mengi ya miradi ya hayakidhi vigezo hivyo kupelekea halimashauri kukosa fedha za miradi ya maendeleo.
Akizungumza kwenye warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Bodi ya mikopo ya serikali za mitaa na Benki ya maendeleo ya (TIB), kwaajili ya kuwajengea uwezo wataalam wa mamlaka za serikali za mitaa juu ya uandishi bora wa maandiko ya miradi Dk. Jilly Maleko amesema kuwa maandiko mengi yanakosa vigezo hivyo miradi mingi kushindwa kutekelezeka.
Amesema kuwa kukosekana kwa vigezo kwa baadhi ya maandiko ya miradi imepelekea miradi mingi kushindwa kupata fedha hali ambayo inapelekea serikali kupoteza fedha nyingi wakati wa kuandaa maandiko.
“Unajua msingi wa upatikanaji wa fedha unatokana na ubora wa mradi na andiko lilivyoandaliwa naamini baada ya warsha hii mtaaza kubuni na kuandaa maandiko ya miradi yanayokidhi vigezo vilivyowekwa” amesema Maleko