27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Matola afichua siri ya kumnyanyasa Zahera

Baada ya kuendeleza ubabe wake dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Seleman Matola amefunguka kuwa ubabe wake dhidi ya miamba hiyo ya Jangwani unatokana na kutumia vema mapungufu yao.

Matola aliiongoza Polisi Tanzania kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Moshi.

Ushindi huo unakuwa tatu kwa Matola dhidi ya Yanga, kwani msimu uliopita aliiongoza Lipuli FC, kushinda michezo miwili mbele ya mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lipuli ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita uliochezwa Machi 16, mwaka huu, kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), uliochezwa Juni 5, michezo yote ikichezwa Uwanja wa Samora, Iringa.

Akizungumza baada ya mchezo wa juzi, Matola alisema mchezo huo ulimwezesha kuindeleza kutengeneza kikosi chake kwa kurekebisha sehemu zenye kasoro.

“Tulikuwa tunahitaji kupata mchezo wa aina hiyo ili kujua ubora wa kikosi chetu, mchezo ulikuwa mzuri na umezidi kutupa njia ya kuona namna tutakavyouanza msimu mpya.

“Siri ya ushindi dhidi ya Yanga ni kutumia mapungufu yao, baada ya kuwafuatilia wanavyocheza kwa muda mrefu, Yanga haikuwa dhaifu, ila kikosi changu kilikuwa bora zaidi yao ndiyo maana tulipata matokeo hayo,”alisema.

Matola alisema Yanga bado ina nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wao wa wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana, kama wataenda kupambana kwa hali na mali.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam, Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1, na wageni wao Township, Uwanja wa Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles