Ramadhan Hassan,Dodoma
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema suala la unyanyasaji wa aina yoyote kwa wachimbaji wadogo wadogo halikubaliki na mmliki yeyote atakaefanya hivyo atakuwa anavunja sheria ya madini na za kazi.
Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 21 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Rhoda Kunchela (Chadema).
Katika swali lake Rhoda amedai kwamba sekta ya madini inaongeza pato kubwa katika uchumi wa nchi ambapo amehoji iwapo serikali ipo tayari kutatua kero kwa wachimbaji wadogo na vibarua ambao wananyanyasika katika migodi mbalimbali hapa nchini.
Akijibu swali hilo Nyongo amesema suala la unyanyasaji wa aina yoyote halikubaliki na mmliki yoyote atakaefanya hivyo atakuwa anavunja sheria ya madini na za kazi.
Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Mombo, David Silinde (Chadema) amehoji kuhusiana na kodi zinazotozwa kwa wachimbaji kuwa nyingi.
Akijibu, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kodi ambazo zimefutwa na Bunge hakuna mbaye anatakiwa kutozwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yule ambaye atamtoza mchimbaji