25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS WA ICC AITAKA MAREKANI KUJIUNGA NA MAHAKAMA HIYO

Rais wa Mahakama ya Kimataifa y Uhalifu ICC ameitolea mwito Marekani kujiunga na kusaidia kazi ya mahakama hiyo.

Wito huo unakuja baada ya Marekani kuongeza mgogoro wake na mahakama hiyo hivi karibuni.

Rais wa ICC Chile Eboe-Osuji amesema wahanga wa zamani, wa sasa na wa baadae wa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita wanahitaji Marekani kuungana na washirika wake na marafiki katika kuridhia mkataba wa Rome ulioanzisha mahakama hiyo.

Marekani haijawahi kujiunga na ICC, ambayo mwendesha mashtaka wake Fatou Bensouda aliwaomba majaji mwaka 2017 kumruhusu afungue uchunguzi katika madai ya uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.

Katika kujibu hilo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, alitangaza wiki mbili zilizopita kwamba watawanyima viza za kuingia Marekani, wanachama wa ICC wanaoendesha uchuguzi wa uhalifu wa kivita dhidi ya wanajeshi wake waliohudumu Afghanistan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles