Serikali ya Ujerumani imesema haitamtambua kama balozi mjumbe wa kiongozi wa upinzani wa Venezuela Juan Guaido aliyejitangaza kuwa Rais wa mpito.
Taarifa hiyo imetolewa na gazeti la Ujerumani Neue Osnabrücker kwa kukariri jibu la Wizara ya Mambo ya Nje baada ya kuulizwa swali na chama cha mrengo wa kushoto.
Hata hivyo Ujerumani itafanya mazungumzo na mjumbe huyo Otto Gebauer lakini hakuna hatua nyingine zinazopangwa kuchukuliwa.
Nchi za Umoja wa Ulaya ikiwa pamoja na Ujerumani zinamtambua kiongozi wa upinzani Juan Guaido kuwa Rais wa mpito wa Venezuela.