26 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Barrick watoa uhakika kumwaga mabilioni

Na Mwandishi Wetu

-Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold anayeshughulikia Afrika na Mashariki ya Kati, Dk. Willem Jacobs, ambaye amemhakikishia kuwa makubaliano ya kampuni hiyo na Serikali yako palepale.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa umma jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Dk. Jacobs amesema hakuna kitakachokuwa tofauti na makubaliano yaliyofikiwa awali, ambayo yaliongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Barrick Gold Corporation Prof. John Thornton.

Sehemu ya makubaliano hayo ni Barrick Gold Corporation kuilipa Tanzania kifuta machozi cha Dola za Marekani milioni 300 (Sh bilioni 682.5).

Mengine ni kuendelea na uwekezaji kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Barrick Gold na mgawanyo wa mapato ya kiuchumi kwa uwiano wa asilimia 50 kwa 50.

Msigwa alisema Dk. Jacobs alikutana na Rais Magufuli ili kumhakikishia makubaliano yaliyofikiwa Oktoba 19 mwaka juzi watayatekeleza kikamilifu, hasa baada ya kuungana katika umiliki, uwekezaji na menejimenti na kampuni kubwa ya uchimbaji dhahabu ya Rand Gold ya Afrika Kusini.

Dk. Jacobs alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kusimamia masilahi ya Watanzania katika rasilimali za nchi yao.

Alisema pamoja na ukweli kwamba Rais Magufuli yupo katika njia sahihi, yeye akiwa Mwafrika anaunga mkono juhudi hizo kwa kuwa ndio mwelekeo sahihi ambao nchi za Afrika zinapaswa kuufuata.

“Mimi ni Mwafrika na sisi sote ni Waafrika, anachokifanya Rais Magufuli ni …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles