25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema wataka polisi imwachie Naibu Katibu Mkuu wao

Asha Bani, Dar es Salaam

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimelitaka Jeshi la Polisi kutoa taarifa rasmi juu ya tukio la kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu na wanachama wengine na kuwaachia huru mara moja.

Jeshi la Polisi mjini Mafinga, mkoani Iringa, linamshikilia Mwalimu baada ya kumkamata mchana wa leo Jumapili Desemba 16, alipokuwa akiwasili kuongoza kikao cha ndani cha chama mjini hapo.

Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, zimeeleza kusikitishwa kwao huku wakilitaka jeshi hilo kuwaachia huru mara moja kwa kuwa hawajaona kosa la wanachama hao.

“Tukio la kukamatwa kwa Mwalimu lilitanguliwa na kitendo cha askari takribani saba kumfuata na kumtoa ndani ya gari kwa nguvu bila kutoa maelezo yoyote ya sababu ya kufanya hivyo.

“Awali, takribani polisi 40 waliokuwa kwenye magari matatu wakiwa na silaha za moto walifika ukumbi wa Mamu ambapo maandalizi ya kikao hicho cha ndani yalikuwa yanaendelea, wakisema kuwa wameagizwa kuzuia kikao hicho na Mkuu wa Wilaya,” amesema Makene katika taarifa yake hiyo.

Aidha, amewataja wengine waliokamatwa pamoja na Mwalimu kuwa ni, Katibu wa Chadema Mkoa wa Iringa, Jackson Mnyawami na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (Bavicha), Mbeya mjini, Jailos Mwaijande ambapo wote wanashikiliwa Kituo cha Polisi Mafinga hadi sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles