32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Afrika wakubaliana kupunguza utegemezi

ADDIS ABABA, ETHIOPIA



VIONGOZI wa Umoja wa Afrika (AU) wamekubaliana kuhusu mageuzi ya kupunguza utegemezi kwa wafadhili.

Wakuu wa nchi za umoja huo pamoja na mawaziri walikutana mjini hapa katika juhudi za kujaribu kufanikisha mageuzi kadhaa ambayo yamekuwa yakipitiwa kwa karibu miaka miwili.

Mwaka 2016 umoja huo ulimpa jukumu mwenyekiti wake, Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuhakikisha mageuzi yanapitishwa, lakini waangalizi walisema muda unakwenda kwa sababu Misri ambayo inapaswa kuchukua uenyekiti, inaonekana kupinga baadhi ya vipengele.

Rais Kagame alipongeza hatua iliyopigwa katika mkutano huo wa siku mbili, ingawa si mapendekezo yote yaliyopitishwa.

Kwa sasa Umoja wa Afrika unategemea ufadhili wa kigeni, na mwaka 2019 utapatiwa asilimia 54 ya bajeti yake ambayo ni jumla ya Dola za Marekani milioni 681.

Umoja huo pia umekubaliana kupunguza idadi ya kamisheni zake kutoka nane hadi sita na kuwasilisha mapato yao kwenye chombo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles