25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli: Upanuzi wa bandari utasaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa mafuta

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Rais Dk John Magufuli amesema upanuzi wa bandari ya Mtwara utasaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa mafuta.

Pia utasaidia yashukie moja kwa moja mkoani mtwara tofauti na sasa ambapo inalazimu  yashushiwe jijini Dar es Salaam kisha yasafirishwe tena kurudi mkoani humo.

Akizungumza na washiriki wa kongamano la kujadili hali ya siasa na uchumi wa nchi ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo Novemba Mosi ambapo amesema bandari ya mtwara itakuwa kituo cha biashara kwa mikoa ya Kusini na nchi za jirani.

“Hatuwezi kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaamvhadi Mtwara karibu kilometa 540 wakati tunaweza kushushia hukohuko na tukayasambaza lakini pia tumeamua kuipanua bandari ya Tanga nayo lazima tuipanue kwa sababu kuna kiwanda kinajengwa cha kuzalisha sarujii ambayo itauzwa ndani na nje ya nchi.

“Tumeamua kuunganisha nchi jirani za Rwanda na Burundi kwa reli ya kisasa ya Stiegler’s Gorge (SGR) ili wanapotumia bandari ya dar kwa ajili ya kusafirisha  bidhaa wapate urahisi nah ii itaiongezea nchi yetu pato kwa kukusanya kodi.

“Huwezi kuongelea kukua kwa uchumi kama hauna umeme wa uhakika na wa bei nafuu tukasema lazima tuwe na umeme wetu na ndiyo maana tukaanza na  mradi wa SGR kwasababu ni umeme wa maji na utakapoanza bei  ya umeme itashuka ”amesema.

Rais Magufuli amesema uwepo wa ndege binafsi ya Dream Liner utasaidia kukuza sekta ya utalii kwasababu watalii wataweza kutoka mataifa mbalimbali na kuja nchini.

“Watalii walikuwa hawaji nchini kwetu kwa sababu hatukuwa na ndege yetu binafsi, huwezi kutumia shirika la ndege la jirani ili kuleta watalii nchini kwako ndiyo maana sisi tukaamua kununua ndege zetu wenyewe na kufufua shirika letu la ndege na lengo kubwa ni  kuinua sekta ya utalii,” amesema.

Aidha Rais Magufuli amesema serikali imenunua rada zitakazofungwa katika jiji la Dar na maeneno mengine ya nchini ili kuongeza ulinzi katika safari za anga na iwe rahisi kujua inapotokea hatari yoyote ile.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles