28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Afya, Costech wazindua matibabu kwa mtandao

Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam



Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wamezindua utoaji wa taarifa za matibabu kwa njia ya mtandao (TanzMED).

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Septemba 28, Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk. Amos Nungu amesema kupitia teknolojia hii, taarifa za magonjwa yote yakiwamo Ukimwi, kisukari, magonjwa ya moyo, kliniki ya watoto, hospitali zilizo karibu na zinazotumia bima ya afya na mengineyo utazipata kupitia mtandao huo.

“TanzMED ilianzishwa baada ya kundi la vijana kuja na wazo la utoaji wa taarifa za matibabu kwa njia ya mtandao, jambo ambalo liliungwa mkono na Costech na kulifanyia kazi, hivyo basi wananchi wataweza kupata taarifa za matibabu, ushauri na maelekezo kupitia mtandao huo,” amesema Nungu.

Aidha, amesema wananchi wanaotumia lugha ya kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi wanaweza kujiunga na mtandao huo ambao utawasaidia kuunganishwa na watalaam wabobezi wa afya ili kupata taatifa hizo, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kwenye huduma za matibabu.

Naye Mtaalamu wa Tehama wa mtandao huo, Mkata Nyoni amesema kwa siku zaidi ya watu 700,000 kutoka ndani na nje ya nchi kwa siku wanaingia kwenye mtandao huo kwa ajili ya kuuliza mambo mbalimbali yanayohusu afya.

“Idadi kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 24 hadi 44 wanaingia kwa siku kutoka ndani na nje ya nchi ili kupata taarifa mbalimbali za matibabu, lengo ni kuwasaidia wananchi waliokua mbali na vituo vya afya ili waweze kupata taarifa sahihi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles