Mwandishi wetu
KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Acacia, imetangaza mpango wa kuhamishia vitengo vyake vingi zaidi nchini na kuongeza matumizi ugavi ya mwaka kutoka kwa watoa huduma wa ndani.
Taarifa ya Acacia iliyotolewa jana inasema kampuni hiyo inaendelea kutekeleza mipango ya kuhamishia vitengo muhimu vinavyohudumia biashara zake nchini ikiwamo ugavi, mauzo na ulipaji wa mishahara.
“Vitengo hivi vitahamishiwa Dar es Salaam au ambako italeta maana zaidi kwa biashara, katika migodi yake iliyopo kanda ya ziwa.
“Mabadiliko haya ni sehemu ya mpango wetu wa muda mrefu ambao tunalenga biashara yetu ya Tanzania iongozwe na kuendeshwa na wafanyakazi wa Tanzania kutokea ndani ya Tanzania,” inasema taarifa hiyo.
Ilisema kwa sasa kati ya mameneja 16 katika migodi yote mitatu ya kampuni hiyo, 12 ni raia wa Tanzania.
“Katika kipindi cha miaka mitano tumepunguza nguvu kazi kutoka nje kwa asilimia 85 na mabadiliko ya sasa yatasababisha kupungua kwa wafanyakazi waliobakia nje ya nchi kwa zaidi ya asilimia 50.
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.