30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

PAPA FRANCIS KUKUTANA NA VIONGOZI KANISA KATOLIKI MAREKANI


Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, kesho anatarajiwa kukutana na viongozi wa Kanisa katoliki la Marekani, kuzungumzia sakata la kashfa ya ngono iliyolikumba kanisa hilo.

Kanisa hilo limekubwa na kashfa hiyo pamoja na vitendo vya kuficha madai hayo yaliyotolewa kwa miaka mingi.

Mkutano huo na Papa Francis, unafanyika huku kukiwa na shinikizo la balozi mstaafu wa Vatican nchini Marekani na askofu Mkuu, Carlo Maria Vigano akimtaka papa huyo ajiuzulu.

Wawili hao wanadai kwamba Papa, miaka mingi iliyopita papa alikuwa akijua ukweli wa taarifa ya aliyekuwa askofu mkuu, Theodore McCarrick wa Washington kumnyanyasa kijana ambaye ni mtumishi wa altare mwaka 1970 pamoja na wanafunzi wengine lakini hakuchukua hatua.

Papa Francis, alimuondoa McCarrick, katika nafasi yake ya ukadinali mwezi Julai.

Kanisa Katoliki nchini Marekani limetikiswa na madai ya miaka mingi kuwa mapadri waliwanyanyasa watoto wadogo katika parokia zao na vitendo hivyo vya uovu vinadaiwa vilifichwa na viongozi wa ngazi ya juu wa kanisa.

Hivi karibuni, washauri wa mahakama katika jimbo la Pennsylvania mashariki, walidai kwamba mapadri 300 wa Parokia mbali mbali nchini humo walikuwa wamewanyanyasa vijana 1,000 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 70.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles