26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

TANESCO YAKAMATA NGUZO 17 ZA VISHOKA

Na MWANDISHI WETU – ARUSHA


SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Arusha, limefanikiwa kukamata zaidi ya nguzo 17 ambazo ziliwekwa na vishoka ambao wamekuwa wakihusisha na wizi wa miundombinu ya umeme katika maeneo ya Murieti na Usa River mkoani hapa.

Akizungumzia mjini hapa leo  Ofisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Dominic Nerrey wakati wa operesheni ya kuondoa nguzo ambazo haziko kwenye ramani ya umeme, alisema vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya umeme vimekuwa vikishika kasi mkoani hapa.

Kutokana na hali hiyo alisema licha ya kuendesha operesheni za kuwakamata vishoka hao bado kumekuwapo na changamoto ya wizi wa miundombinu ya umeme.

“Tunawasaka vishoka na wezi wote wa miundombinu ya umeme kwani hasa ndiyo wamekuwa wakisababisha kukosekana kwa huduma ya uhakika ya umeme. Tanesco tunawataka watu wote waliofanya vitendo hivi viovu kujisalisha mara moja na wale watakaokaidi tutawafikisha kwenye mikono ya sheria.

“Jamii ni lazima itambue kwamba suala la ulinzi wa miundombinu ni wajibu wa kila Mtanzania kwani unapowaona watu waovu ambao si watumishi wa Tanesco au una shaka nao tafadhali toa taarifa kwetu nasi tunashughulika nao kwa mujibu wa sheria,” amesema Nerrey

Amesema kwa kipindi cha miezi sita wamefanikiwa kubaini kuwa zaidi ya nguzo 17 ziliwekwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo ambayo hayako kwenye ramani ya umeme.

Akizungumzia hali hiyo, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Henry Mhina, amesema suala la uwepo wa vishoka imekuwa inachangiwa na wananchi ambao wamekuwa wakikwepa kupata huduma kwenye ofisi za Tanesco na badala yake wanawatumia watu ambao hawajuni misingi ya umeme kwa mujibu wa sheria.

Amesema umefika wakati wa wananchi wakatae kuunganishiwa umeme kienyeji na badala yake wawe na wanakwenda Tanesco ambao watahudumiwa kwa wakati ikwiamo kuunganishiwa umeme kwa mujibu wa utaratibu.

Alitaja uwepo wa sababu mbalimbali zinazofanya kuendelea kwa ongezeko la vishoka hao ikiwemo uwepo wa miradi ya umeme inayotekelezwa katika nyakati tofauti ikiwemo Mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja Mkoa wa Arusha, Said Mndeme, amesema kuwa wahujumu miundombinu ya Tanesco wamekuwa wakilitia hasara kuwa shirika hilo ikiwamo kuharibu laini za umeme ambao zimekuwa zinapeleka huduma za umeme kwa wananchi.

Amesema hali hiyo imekuwa ikisababisha wananchi hao  ambao maeneo yao wamehujumiwa na wezi hao wa miundombinu ya umeme kupata umeme mdogo kwa baadhi ya maeneo wanayotoa huduma hiyo.

Wakizungumzia hali hiyo mmoja wa wananchi wa Muriet, Mery Maliwa na Ndetakashulo Ismail, wamesema wanashangazwa na hali hiyo huku vishoka hao wakienda kwenye maeneo hayo nyakati za usiku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles