30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI KUNUFAIKA KINGA YA MINYOO, KICHOCHO

Na WAANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


JUMLA ya wanafunzi 678,000 wa shule za msingi jijini Dar es Salaam wanatarajia kunufaika na kinga ya magonjwa ya kichocho, minyoo na mabusha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo jana, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Grace Maghembe, alisema wanafunzi hao watatoka katika shule 708 za Serikali na binafsi.

Alisema kinga hiyo itatolewa chini ya mpango maalumu wa taifa wa kushughulikia magonjwa yasiyopewa kipaumbele ambayo hufanyika kila mwaka mara moja.

“Kinga hii huzuia kupata kansa ya kibofu cha mkojo, kichocho, mabusha, matende na minyoo, hivyo ni vyema wazazi wakawaruhusu watoto wao wapatiwe kinga hiyo,” alisema Grace.

Alisema kinga hiyo itatolewa kwa kuzingatia urefu pamoja na uzito.

Aliwataka wananchi kujenga utamaduni wa kupata kinga mapema kabla ya kusubiri ugonjwa kulipuka.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema katika mkakati huo walimu 1,500 na watoa huduma 392 walipata mafunzo ya kuelimisha umuhimu wa kinga hiyo.

Alisema ni vyema jamii ikaachana na imani potofu wakati mradi huo ukitekelezwa kwani wengi wamejenga hisia kuwa endapo watapata kinga hiyo watakosa uzazi hapo baadaye.

Habari hii imeandaliwa na CHRISTINA GAULUHANGA, MAGRETH MSANGI Na FRANK KAGUMISA (TURDACO)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles