30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Afande Sele: Wanaonipiga zengwe wana hofu nitawashinda

aFANDE seleeAKIWA katika maandalizi ya kuanza harakati za kuomba kura kwa wananchi wa Morogoro Mjini anapogombea nafasi ya ubunge mkoani humo, mkali wa hip hop nchini, Seleman Msindi ‘Afande Sele’, amejikuta akiwekewa pingamizi lenye madai kwamba hajui kusoma na kuandika.

Afende Sele alisema ameshangazwa na pingamizi hilo lisilo na maana katika siasa kwa kuwa haliwashtui wapigakura wake kwa kuwa wanamfahamu vizuri ngazi zote za shule alizopitia.

“Nimeshangazwa nilipoitwa kwa mkurugenzi Manispaa ya Morogoro mjini akaniambia nimewekewa pingamizi na chama kimoja wapo mkoani huko wakidai sijui kusoma na kuandika, sasa huo si upofu wa kisiasa, ninachojua ni kwamba wananiogopa hivyo wanahangaika kuniwekea vizingiti vingi,” alisema Afande Sele.

Aliongeza kwamba, pingamizi hizo hazina faida kwa wananchi wanaotaka wawaongoze kwa kuwa wanamfahamu na ana elimu nzuri inayomwezesha kuishi maisha ya kawaida kama wananchi wengi wa mkoa huo.

“Kuchafuana huko kusiko na maana hakujengi mkoa wetu wala hakuwakwepeshi wananchi wa Morogoro mjini kukwepa kupiga kura, watapiga kura na kwa kuwa nina uhakika wananifahamu na wanataka kiongozi aliyekaribu nao na anayejua shida zao, sina shaka na wanaonichafua kwa kuwa hofu yao haitowaisha hadi nitakaposhinda,” alieleza Afande.

Afande ni mmoja wa wasanii watakaogombea ubunge kwa mwaka huu wa 2015 wengine ni Joseph Haule ‘Profesa Jay’ anayegombea ubunge jimbo la Mikumi (Chadema), Irene Uwoya viti maalumu Tabora (CCM), Kingwendu anayegombea Kisarawe kupitia (CUF), Mohammed Mwikongwe ‘Frank wa Kaole’, anagombea Segerea kupitia (ACT).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles