27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

RC SINGIDA AFUNGA KLABU YA USIKU

Na SEIF TAKAZA-SINGIDA


MKUU wa Mkoa (RC) wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, ameagiza klabu ya usiku iliyopo jirani na Shule ya Msingi Ipembe, mjini hapa ifungwe kwa sababu inachangia kuharibika kwa mazingira ya shule hiyo.

Dk. Nchimbi alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Pentekoste la FPCT lililopo Kata ya Ipembe, mjini hapa.

Alisema klabu hiyo ya usiku imejaa vituko vingi, vikiwamo vya wanawake kuifanya shule hiyo kuwa kituo cha kufanyia ukahaba.

“Sasa kwa kuwa klabu hiyo iko jirani na shule ya msingi, mipira ya kujamiiana iitwayo kondom, imekuwa ikitupwa ovyo hapo shuleni, jambo ambalo hatuwezi kulivumilia kwa sababu inaharibu pia mazingira.

“Hatuwezi kuwa na night klabu au baa ambazo zinakuwa kituo cha makahaba kufanya biashara yao ya kuuza miili katika maeneo ya shule.

“Kwa mamlaka niliyonayo, uongozi wa hiyo night klabu, usicheze na Serikali yangu kwani haitavumilia vitendo hivyo isipokuwa itaruhusu biashara zozote zilizo halali na siyo biashara za kuuza miili,’’alisema Dk. Nchimbi.

Katika hatua nyingine, Dk. Nchimbi aliwataka watumishi wa umma waliopo kwenye madhehebu mbalimbali ya dini, kuonyesha hofu ya Mungu wakati wakitekeleza majukumu yao.

“Watumishi wa Serikali wapo kila nyumba za ibada za madhehebu mbalimbali jambo linaloifanya Serikali na madhehebu ya dini, kuwa kwenye mnyororo mmoja wa kuwatumikia wananchi.

“Kwa hiyo, mtumishi kama nesi na daktari anapokuwa akitimiza majukumu yake, ahakikishe anamtanguliza Mungu Mungu ili aweze kufanya kazi kwa mafanikio,” alisema.

Naye Askofu Mstaafu wa Kanisa la Pentekoste, Dk. Paulo Samwel, alisema kanisa lake linashirikiana kwa karibu na Serikali katika juhudi za kuwahimiza waumini na wasiokuwa waumini, washiriki shughuli za maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles