30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

HOFU YATANDA KWA WANAOISHI NA ALBINO

Na Derick Milton -BARIADI

ALBINO na familia zao katika Wilaya ya Bariadi  wanaelezwa kuendelea kuishi kwa hofu ya kuuawa au kukatwa vioungo vyao kutokana na kuendelea kutokea kwa matukio hayo.

Unyanyapaa unaofanywa na wananchi dhidi ya watu wenye ualbino katika wilaya hiyo, nao uimeendelea kusababisha watu hao kuendelea kuishi katika hofu.

Hayo yalisemwa na viongozi vijiji na kata wa wilaya hiyo katika mafunzo ya kupiga vita mauaji ya watu wenye ualbino yaliyofanyikia mjini Nkololo.

Mafunzo hayo yaliendeshwa na Shirika la Mass Media Bariadi kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Sociaty.

Viongozi hao kutoka kata za Nkololo, Mwaumatondo na Ihusi, walisema   katika Kata ya Mwaumatondo, hofu kwa watu hao ni kubwa kwa vile kutokana na    tukio la kuuawa  mtu mwenye ualbino mwaka 2014.

“Bado hofu kwa watu wenye ualbino na familia zao ni kubwa … wanaishi huku kwa hofu ya kuuawa au kukatwa viungo vyao  hasa kwenye kata ya Mwaumantondo ndiyo kubwa zaidi,” alisema Kellya Sabale mtendaji wa kijiji cha Bubale.

Viongozi hao waliomba serikali   na wadau wengine kuimarisha kamati za ulinzi na usalama za vijiji na kata katika kutambua majukumu yao ya kuhakikisha wanawawekea ulinzi wa kutosha wananchi wao.

“Kamati za ulinzi na usalama za vijiji na kata nyingi hazifanyi kazi, haziko hai, wajumbe wengi hawana elimu ya majukumu yao.

“Tunaiomba serikali kutoa elimu kwa watu hawa ili hofu hii kwa wenye ualbino iweze kuisha kwa kuwekewa ulinzi wa kutosha,” alisema Bahame Maduhu Mwenyekiti Kijiji cha Nkololo.

Mratibu wa mradi wa kupiga vita mauaji ya watu wenye ualbino kutoka Mass Media, Frank Kasamwa, alisema   ikiwa kamati za ulinzi na usalama  za vijiji na kata zitafanya kazi inavyotakiwa mauaji hayo hayatakuwapo.

“Kamati hizi ndizo zenye wajibu mkubwa wa kuhakikisha wanawalinda wananchi wake.

“Ikiwa zitaimalrshwa na kupewa elimu, matukio hayatakuwapo,” alisema Kasamwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles