32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

DIWANI, MWENYEKITI KORTINI KWA KUCHOMA MALI ZA MWEKEZAJI

Na TWALAD SALUM-MISUNGWI

DIWANI wa Kata ya Mabuki, Nicodemas Ihano (CCM) na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanangwa kilichopo wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza, Faustine Malago (CCM), wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuvunja  nyumba, kuiba na kuchoma  moto mali za mwekezaji.

Ihano ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Wilaya ya Misungwi na wenzake watatu, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya hiyo na kusomewa hati za mashtaka matatu ambapo walikana mashtaka yanayowakabili na wote wako nje kwa dhamana.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Russy Mkisi, Mwendesha Mashtaka wa polisi, Ramsoney Salehe, aliiambia Mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao kwa  pamoja Oktoba 24, mwaka huu saa 7.00 mchana kwenye Kijiji cha Mwanangwa  eneo la machimbo ya madini ya almasi, walikula njama na kuvunja  nyumba na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani  ya Sh milioni 2.8.

Salehe alisema tuhuma nyingine zinazowakabili washtakiwa hao ni kuchoma moto nyumba na magari mawili vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 170.8 mali ya Badar Sudi mkazi wa Shinyanga ambaye ni mwekezaji  na mchimbaji wa kati wa madini ya almasi katika Kijiji cha Mwanangwa.

Watuhumiwa wote walikana mashtaka yanayowakabili ambapo walikidhi masharti ya dhamana iliyowataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wenye mali isiyohamishika na wote wako nje kwa dhamana ya Sh milioni 5 kila mmoja.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Stephano Bengwe (32) na  Herddius Gwido (40), wote wakazi  wa Kijiji  cha  Mabuki, ambapo Hakimu Mkazi Mfawidhi, Russy Mkisi, aliahirisha kesi hiyo ambapo itatajwa tena Novemba 14, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles