WASHINGTON, MAREKANI
NYOTA wa muziki nchini Marekani, Ciara Harris, juzi aliwafariji mashabiki wake wagonjwa baada ya kuwatembelea katika hospitali ya watoto ya Seattle na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Ciara aliungana na mume wake, Russell Wilson na mtoto wao, huku wakiwa na zawadi mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa. Siku hiyo Ciara alikuwa anasherehekea kutimiza miaka 32 ya kuzaliwa kwake.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, aliwashukuru viongozi wa hospitali hiyo kwa kumpa nafasi ya kuwafariji wagonjwa.
“Ninaamini kila sehemu kuna mashabiki wangu, nikaona bora siku yangu ya kuzaliwa nikaungane na baadhi ya mashabiki ambao ni wagonjwa, lengo kubwa lilikuwa ni kuwafanya wawe na furaha, japokuwa ni wagonjwa, tunawapenda wote,” aliandika Ciara.