Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Raheem Nanji ‘Bob Junior’, ameisifu sauti yake na kudai kuwa, hakuna msanii anayeweza kupangilia mashairi kama yeye.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, msanii huyo, ambaye ameachia wimbo wake mpya unaojulikana kama ‘Longo longo’, alisema anajikubali, ndiyo maana ana imani kazi anazofanya zitafanya vema.
Alisema amekuwa kimya muda mrefu, hivyo amerejea kwenye tasnia nzima ya muziki kuendeleza kipaji chake alichobarikiwa na Mungu.
“Nimerudi kuendeleza pale nilipoishia, matumaini yangu nitarudisha kiwango na hadhi yangu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,” alisema Bob Junior.