25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 9, 2024

Contact us: [email protected]

DAXO CHALI AWATEMA WASANII WAKE

Na CHRISTOPHER MSEKENA

MTAYARISHAJI wa muziki na mdogo wa prodyuza maarufu nchini, Marco Chali, kutoka studio za Mj Records, Daxo Chali, amesema utovu wa nidhamu ndio umefanya aache kuwasimamia kimuziki wasanii wa kike, Haitham Kim na Nini.

Daxo Chali, ambaye ametengeneza nyimbo nyingi, ikiwamo Dume Suruali ya Mwana Fa na Vanessa Mdee, ameliambia MTANZANIA kuwa, anafurahi kuona wasichana hao wamefahamika, lakini amelazimika kuacha kuwasimamia kutokana na kukosa nidhamu.

“Nimeamua kuacha kuwasimamia Haitham na mwenzake Nini ili kutoa nafasi kwa wadau wengine kuendelea kuwasimamia, juhudi zangu zimewafikisha hapo, kwa yeyote akayaependa awaendeleze tu ni wasanii wazuri, unajua nidhamu ni kitu muhimu kwa msanii na inapokosekana kazi haziweze kufanyika,” alisema Daxo, mtoto wa mwisho kwenye familia ya watayarishaji muziki Marco Chali, Biff Chaa na Zaa Chaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles