29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA MMILIKI LACKY VINCENT YAAHIRISHWA

Na JANETH MUSHI- ARUSHA

KESI inayomkabili mmiliki wa Shule ya Msingi, Lucky Vincent, Innocent Moshi anayekabiliwa na makosa ya usalama barabarani imekwama kuendelea kusikilizwa jana kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwapo mahakamani.

 

Moshi pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Longino Nkana,wanakabiliwa na mashitaka matano likiwamo la kusafirisha wanafunzi bila kuwa na vibali muhimu.

 

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Jasmine Abdul, Wakili wa Serikali aliieleza mahakama hiyo kuwa Jamhuri inao mashahidi wawili hivyo wanaomba kesi hiyo kesi hiyo namba 78 ya mwaka huu,  iendelee kusikilizwa.

 

Hakimu Abdul alisema kutokana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Desderi Kamugisha, aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo kutokuwapo mahakamani hapo, kesi hiyo itaahirishwa hadi Novemba 16 mwaka huu.

 

Mmoja wa mashahidi waliotarajiwa kutoa ushahidi wao jana ni pamoja na Mohamed Matumula kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar Insurance.

 

Mashahidi wengine ni pamoja na mwanafunzi mmoja Wilson Tarimo, aliyenusurika katika ajali hiyo ya basi iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.

 

Wengine ni Songoyi Jilala, Inspekta Shukrani, G 4130 PC Mwita, Ignatus Paula, Koplo Saada na E.4312 PC Mugobe, ambao wote ni askari wa usalama barabarani Arusha na Karatu, Leonidas Gerald (Morombo) na Hamis Omary (Sombetini).

 

Waliokwishatoa ushahidi ni D 9967 Koplo Hamad kutoka Karatu na  Afisa Kazi kutoka Idara ya Kazi Arusha,Wilfred Mdumi na Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Arusha(RTO),Nuru Suleiman,ameieleza mahakama kuwa basi lililosafarisha wanafunzi lilikuwa na leseni ya usafirishaji abiria.

Katika kosa la kwanza,  Moshi anatuhumiwa kufanya biashara ya usafirishaji abiria bila kuwa na leseni ambapo kati ya Desemba 12 mwaka jana hadi Mei 6 mwaka huu alitumia gari Mitsubishi Rossa T. 871 BYS kubeba wanafunzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles