32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

MOBETTO AVAANA NA VERA SIDIKA

Na SWAGGAZ RIPOTA

BADO stori za mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mzazi mwenzake mjasiriamali Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’  hazijapoa. Fujo za kutosha mitandaoni.

Ni mfululuzo wa matukio yaliyoanza na Diamond kukiri wazi kuwa alipata kuwa na uhusiano na mwanamitindo Hamisa Mobetto na kuzaa naye mtoto Dylan a.k.a Abdlullatif.

Kukubali kwa Diamond kumekuwa kama kete kwa Hamisa ambaye ameonekana akitamba mitandaoni kwa matukio mbalimbali yakimhusisha na Diamond na mtoto wao Dylan huku wakati mwingine hata Zari.

Hamisa ambaye hivi karibuni ameweka wazi kuwa alikuwa kwenye uhusiano na Chibu kwa miaka tisa mpaka wamepata mtoto (Dylan), siku mbili hizi alikuwa jijini Nairobi nchini Kenya kwenye klabu moja alipoalikwa na huko akanisanua na kuvaana na mwanamitindo Vera Sidika.

AMCHOKONOA VERA SIDIKA

Wakati Mobetto anapiga misele jijini Nairobi, alikutana na mrembo Vera Sidika ambaye na yeye alikuwa matembezini akiendesha gari ndogo la kawaida sana.

Ndani ya gari alilokuwa amepanda, Mobetto alikuwa na mshkaji wake Vera Sidika anayeitwa Cuppy ambapo walishusha vioo vya magari yao na kusalimiana.

Wakati marafiki hao wakisalimiana, Mobetto aliyekuwa ameketi kiti cha nyuma cha gari la Cuppy alikuwa anamrekodi video mrembo huyo wa Kenya (Vera Sidika) bila ya Vera mwenyewe kugundua kitendo hicho.

VIDEO YAIBUA UGOMVI

Baada ya muda kupita, Hamisa Mobetto aliiweka ile video ya Vera kwenye mtandao wa SnapChat na kuweka vi-emoji vinavyo onyesha love.

Kitendo hicho kilimchukiza mno Vera, hakupenda na akamjibu kupitia SnapChat kuonyesha hasira zake kwani ilionekana vibaya.

HAMISA AMTAJA TENA ZARI

Moja na matusi ambayo Vera alimtukana Mobetto ni kuwa ametoka Tanzania kwenda Kenya kujiuza kwa wanaume ambao yeye (Vera) anawafahamu kwani wakishatoka na Mobetto huwa wanamwambia.

Alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa hata sherehe ya mtoto wake Prince Dully au Daylan, kuna kidume cha Kenya kiligharamia.

Mebetto alijibu tuhuma hiyo kuwa Vera anasumbuliwa na wivu kwa kuwa yeye (Mobetto) amekwenda nchini kwake na kupata dili la pesa ndefu kwenye klabu moja na kuhusu hao wanaume, Mobetto akasema yeye anatafutwa na wanaume na siyo yeye kuwatafuta.

Hamisa aliongeza kwa kumtaja kimafumbo Zari ambaye ni rafiki mkubwa wa Vera kwa kusema: “Wewe kuwa rafiki wa yule mwingine (Zari) haimaanishi uongee mabaya kuhusu mimi, usinifanye nikudhalilishe sababu unajua nina ushahidi.”

Vera alirudi tena SnapChat na kumjibu haikuwa kipindi sahihi kwa Mobetto kumposti yeye (Vera) wakati huu ambapo Zari ana ugomvi wa Mobetto kwa kutengeneza chokochoko.

WAVUANA NGUO

Mtandao wa SnapChat ulichafuka kwani wawili hao walivuana nguo kwa kutupiana maneno machafu zikiwa ni pamoja kashfa mbalimbali.

Vera alimkejeli Mobetto kwa kwa kuwa mchepuko wa Diamond kwa miaka kumi, kuzaa watoto wawili na wanaume tofauti, kuwatumia watoto wake kama ATM Machine akaweka wazi kuwa yeye (Vera) anajiuza kwa kusema mafanikio hayaambukizi kwa kujihusisha na mambo ya  mapenzi.

Mobetto naye hakukaa kimya, akasema watoto wake wanamnyima usingizi Vera. Hamisa pia akaweka ushahidi wa screenshot zikionyesha Vera ndiye aliyeanza kujipendekeza kwake (Mobetto) kwa kutaka apate mashabiki kwenye ukurasa wake wa Instagram yake kutoka hapa Tanzania mwaka 2014.

Mtiti huo uliendelea kwa muda mrefu huku wawili hao wakiendelea kurushiana maneno ya kuudhi kwenye kurasa zao katika mtandao wa SnapChat.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles