27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MWINGINE AJIFUNGUA ANGANI

IWAPO unahitaji huduma za aina yake za daraja la kwanza bila kujali kama umelipia tiketi ya daraja la ‘walalahoi’ huku ukijichia na kuhudumiwa kama mfalme, nenda tu ukajifungue ukiwa kwenye ndege.

Ndege moja ya Shirika la Ndege la Uturuki ililazimika kukatisha utoaji wa huduma za vinywaji kwa abiria waliokuwamo katikati ya safari kutoka Conakry nchini Guinea kwenda mjini Ouagadougou, Burkina Faso.

Wahudumu wa ndege hiyo waliamua kuchukua hatua hiyo baada ya mmoja wa abiria, Nafi Diaby alipojifungua ndege ikiwa angani.

Kwa sababu hiyo ikabidi wasitishe huduma hizo ili wazihamishe kwa Diaby na abiria mpya, yaani kichanga wa kike.

Huduma hizo zilizohamia daraja la kwanza zilienda sambamba na kusherehekea kwa ujio wa abiria huyo aliyepewa jina la Kadiju, wakati ndege ikiwa umbali ya futi 42,000 au mita 12,800.

Abiria nao walisaidia kuzaliwa kwa mtoto huyo, muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka Conakry, ikielekea Istanbul nchini Uturuki kupitia Burkina Faso.

Mama na mtoto wake huyo walipelekwa hospitali wakati ndege hiyo aina ya Boeng 737 ilipotua Ouagadougou.

Wote waliripotiwa kuchoka lakini walikuwa na afya nzuri.

Wahudumu waligundua kuwa mwanamke huyo Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa kujifungua.

Hapo ndipo walichukua hatua ya kumsaidia kujifungua ndege ikiwa safarini.

Wakati wataalamu wa afya wakisema kwa ujumla ni salama kwa mwanamke mjamzito kusafiri kwa ndege kabla ya kufikisha wiki 36 za ujauzito, Shirika la Ndege la Uturuki huruhusu mwanamke kupanda ndege akiwa kati ya wiki 28 na 35 akiwa tu na kibali cha daktari.

“Mwanamke huyu alikuwa katika maumivu makali,” mmoja wa wafanyakazi wa ndege hiyo, Bouthayna Inanir alisema na kichanga kikawa kitini, hii ni sehemu ngumu na ilibidi nimchukue mtoto. Nilimchukua na kumpatia mama yake.

“Karibu kwenye ndege binti mfalme,’ yalisomeka maandishi katika picha ya wafanyakazi wa ndege wakionekana na furaha wakijumuika na mtoto na mama yake katika picha walizotuma katika mitandao ya jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles