32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

CONTE: NILIKUWA ‘NATESTI’ MITAMBO

LONDON, ENGLAND

BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England kukubali kichapo cha mabao 3-2 kwenye uwanja wa nyumbani wa Stamford Bridge dhidi ya Burnley, kocha wa mabingwa hao, Antonio Conte, amedai alikuwa anajaribu wachezaji wake.

Kocha huyo amesisitiza kuwa hana wasiwasi na matokeo hayo ya mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa ligi, atahakikisha anakiweka sawa kikosi hicho kwa ajili ya kutetea ubingwa msimu huu.

Kocha huyo katika kipindi hiki cha usajili amefanikiwa kufanya usajili wa wachezaji wanne huku akitumia kiasi cha pauni milioni 129, lakini amesema kikosi chake kimekosa wachezaji wenye uzoefu kama vile John Terry na Nemanja Matic ambao wameondoka katika kipindi hiki cha usajili.

Conte aliongeza kwa kusema kucheza huku timu ikiwa pungufu imechangia kushindwa kufanya vizuri baada ya Gary Cahill na Cesc Fabregas kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu.

“Wachezaji wangu walikuwa wanajaribu kuonesha ubora wao, lakini mambo yalikuwa tofauti na vile tulivyotarajia, hata hivyo sina wasiwasi kwa kuwa nilikuwa natesti mitambo yangu na sasa nipo tayari kupambana na wachezaji nilionao.

“Narudia kwa kusema kwamba kitu muhimu kwa sasa ni kuangalia jinsi gani tutajiweka sawa, hivyo tunatakiwa kuboresha baadhi ya mambo wakati wa mazoezi hakuna la zaidi,” alisema Conte.

Kocha huyo amekubali kuwaachia wachezaji wake wazoefu kuondoka, Terry ambaye alikuwa anacheza nafasi ya ulinzi wa kati, kiungo Matic, kipa wake, Asmir Begovic, aliyejiunga na kikosi cha Bournemouth, wakati huo mfungaji wao bora msimu uliopita, Diego Costa, akiambiwa yupo huru kuondoka kwa kuwa hayupo kwenye mipango yake msimu huu.

Wakati huo wachezaji aliowasajili kipindi hiki ni pamoja na kiungo kutoka Monaco, Tiemoue Bakayoko, mshambuliaji kutoka Real Madrid, Alvaro Morata, beki kutoka AS Roma, Antonio Rudiger na aliyekuwa kipa wa Manchester City, Willy Caballero.

Dirisha la usajili bado lipo wazi hadi Agosti 31 mwaka huu, hivyo kocha huyo ameweka wazi kwamba kuna uwezekano wa kuongeza wachezaji wengine ili kuboresha kikosi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles