32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGOZI EAC WAMPONGEZA UHURU

Na mwandishi wetu – dar es salaam

RAIS Uhuru Kenyatta amemiminiwa pongezi na viongozi wa nchi za Burundi, Rwanda, Tanzania na maeneo mengine duniani.

  1. JOHN MAGUFULI

Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli aliandika kupitia ukurasa wake wa twitter: “Nakupongeza Ndugu Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema.”

YOWERI MUSEVENI

Rais Yoweri Museveni wa Uganda alitoa taarifa kwa umma akisema:  “Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Uganda na mimi kama Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, napenda kutoa pongezi kwa ushindi uliopata wa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya.

“Kuchaguliwa kwako tena ni ishara ya kuaminiwa na wananchi wa Kenya na kuthamini juhudi zako za kuleta maendeleo nchini mwako na ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano iliyopita.”

EDWARD LOWASSA

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ambaye alishiriki kumpigia kampeni Uhuru katika uchaguzi huu, aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter: “Hongera sana kwako ndugu yangu Uhuru Kenyatta kuchaguliwa tena, Wakenya wamezungumza kwamba bado wana imani na uongozi wako, na mipango kwa ajili ya Kenya. Mungu ibariki Afrika Mashariki.”

PIERRE NKURUNZIZA

Akitumia ukurasa wake wa twitter, Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza naye aliandika: “Kwa niaba ya wananchi wa Burundi, napenda kukupongeza rais mteule, Uhuru Kenyatta na wananchi wote wa Kenya. Nategemea tutaendelea kuimarisha ushirikiano wetu.”

PAUL KAGAME

Paul Kagame wa Rwanda alimpongeza Uhuru Kenyatta kwa kuandika: “Hongera sana kaka yangu Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena na imani ya wakenya waliyonayo kwako.”

FREEMAN MBOWE

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, naye alimpongeza Uhuru kupitia katika ukurasa wake wa Twitter.

“Kwa niaba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo – Chadema na wapenda demokrasia wa Tanzania, natoa pongezi kwa kuchaguliwa tena kuongoza Kenya. Pongezi zaidi kwa wananchi wa Kenya kwa uchaguzi wa uwazi na haki. Mungu ibariki Jumuiya ya Afrika mashariki.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles