Hatua hiyo inakuja baada ya wakazi wa eneo la Gunjur, kusini mwa mji Mkuu wa Banjul kulalamika kuwa mamia ya samaki wamekuwa wakifa katika eneo hilo la bahari tangu kampuni hiyo ya Golden Lead ilipojenga kiwanda cha kusindika samaki katika mji huo mwaka 2016.
Wanasema watu ambao wamekuwa wakiogelea katika eneo hilo wamekuwa wakidhurika na kupata matatizo ya kiafya.
Kampuni ya Golden Lead imepinga tuhuma hizo.
Kampuni hiyo ilikubaliana kumaliza suala hilo nje ya mahakama na Mamlaka ya taifa ya Mazingira nchini Gambia mwezi uliopita. Source BBC