27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘WOGA WA MADARAKA KIKWAZO KWA VIONGOZI’

Na JOHANES RESPICHIUS

Woga wa kupoteza madaraka umetajwa kuwa changamoto kubwa inayokandamiza haki ya kujieleza kwavile  viongozi wamekuwa hawataki kukosolewa na mtu yeyote wanapokuwa madarakani.

Hayo yalibainishwa katika semina ya Jinsia na Maendeleo (GDSS) iliyoandaliwa na Mtandao ya Jinsia Tanzania (TGNP) kuhusu haki wa kujieleza na Mwanasheria wa Dawati la Utetezi na Katiba wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Happyness Michael.

Alisema woga wa kupoteza madaraka umekuwa changamoto kubwa kwa haki wa kujieleza ambako viongozi wamekuwa hawataki kukosolewa na mtu yeyote wanapokuwa madarakani.

“Kutokana na hali hiyo ndiyo maana tumekuwa tukishuhudia matukio mbalimbali ya kukamatwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakionekana kukosoa kwa namna moja au nyingine utawala uliopo madarakani.

“Tumeona baadhi ya wasanii wakikamatwa na kutekwa kwa kile kinachodaiwa kuimba nyimbo ambazo zinakosoa Serikali na viongozi wake.

“Pia Yeriko Nyerere, amekuwa akikamatwa kutokana na ujumbe ambao amekuwa akiziandika kwenye mitandao ya  jamii jambo ambalo limekuwa likikandamiza haki hii ya msingi,” alisema Happyness.

Alisema kuna mambo mengi yanayoikabili haki za watu kujieleza kama vile mamlaka makubwa aliyopewa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwenye Sheria ya Huduma  kwa Vyombo vya Habario  ya mwaka 2016, kwa hatua yake ya kulifungia Gazeti la Mawio  jambo ambalo linaathiri uhuru wa kujieleza.

“Pia sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015, tumeona watu wanaokamatwa ni wale  wanaojieleza hasa  wanapofanya jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linahoji utendaji wa utawala uliopo madarakani,” alisema Happyness.

Alisema upungufu huo ndiyo ulisababisha  LHRC kufungua kesi za katiba kuhusu Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 katika Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mwanza na Mahakama ya Afrika Mashariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles