30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

SUMAYE AJIONDOA CRDB KUIMARISHA CHADEMA

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Pwani, Frederick Sumaye

 

 

Na ELIYA MBONEA, ARUSHA

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Pwani, Frederick Sumaye, ametangaza kujiuzulu ukurugenzi wa Bodi ya Benki ya CRDB, akisema anataka apate fursa zaidi kuimarisha chama chake.

Kiongozi huyo wa zamani ambaye sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitangaza uamuzi huo wakati wa Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa CRDB uliofanyika mkoani Arusha jana.

Sumaye aliyepigiwa kura kwenye nafasi hiyo ya ukurugenzi miaka mitatu iliyopita, alisema kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake, aliona ni vyema asigombee tena nafasi hiyo.

“Nilipata shida kidogo kwenye uamuzi huu, watu watawaza nini, naomba niwaambie hakuna tatizo, benki yetu tunaendelea kuwa imara. Zipo sababu

zangu binafsi ambazo nimeona nizitekeleze ili kuendelea kulinda masilahi mapana ya benki yetu na Watanzania,” alisema Sumaye na kuongeza:

“Nimekuwa na shughuli nyingi za kisiasa ambazo zinanichukulia muda mwingi sana, hivyo nikaona nikiendelea kuwa mjumbe wa bodi nitakuwa

mjumbe asiyehudhuria vikao na hili si jambo jema.

 “Kwa hali hii ya kisiasa, sikutaka kabisa benki hii ninayoiheshimu ije ifikiriwe kisiasa, kwamba shughuli zangu za kisiasa sikutaka zihusishwe na benki. Hivyo nimelazimika kutanguliza masilahi makubwa ya benki yetu inayofanya kazi kubwa ya kuinua uchumi wa nchi.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema utendaji wa benki hiyo mwaka 2016 uliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya ghafla ya mazingira ya uendeshaji yaliyoathiri hali ya ukwasi na usimamizi wa vihatarishi vya mikopo.

Dk. Kimei alizitaja baadhi ya sera zilizoathiri mazingira ya biashara kuwa ni  udhibiti wa sera ya fedha uliojumuisha hatua za kubana matumizi na kuongeza usimamizi katika ukusanyaji wa kodi.

 “Jitihada hizi zilienda sambamba na kuwatambua na kuwaondoa kwenye mfumo wa malipo wa Serikali wafanyakazi hewa na wanafunzi ambao

hawakustahili kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

“Lakini pia kuhamishwa kwa amana za mashirika ya umma ambazo zaidi ya Sh bilioni 700 zilipelekwa Benki Kuu kwenye akaunti moja ya Hazina,” alisema Dk. Kimei.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles