27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

PANDA SHUKA YA SIKU 120 ZA LEMA GEREZANI

Na JANETH MUSHI-

-ARUSHA


LEMA alikamatwa Novemba 2, mwaka jana mjini Dodoma nje ya viwanja vya
Bunge na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Novemba 4
mwaka jana akikabiliwa na kesi mbili namba 440 na 441 za uchochezi
dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Katika kesi ya kwanza ya jinai namba 440, anadaiwa kati ya Oktoba 22
mwaka huu maeneo ya Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro, katika mkutano
wa hadhara alitoa maneno yenye kuleta tabaka miongoni mwa jamii kwa
kutoa matamshi yenye chuki, kuibua nia ovu kwa jamii.

Katika kesi ya pili namba 441, alidaiwa kwamba, Oktoba 23, mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa, Lema  alitoa maneno kuwa: “Kiburi cha Rais
kisipojirekebisha, Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, nimeota  Mwaka 2020
haitafika Mungu atakuwa ameshamchukua maisha yake.”

“Rais ana kiburi, Rais kila mahali watu wanaonewa, wafanyakazi wa
Serikali hawana amani, wafanyabiashara hawana amani, watu
wananyanyaswa.”

Lema alikosa dhamana baada ya mawakili wa Serikali kuweka pingamizi.

Novemba 11, alishindwa kupewa dhamana licha ya mahakama hiyo kusema
dhamana iko wazi baada ya Mawakili wa Serikali kuwasilisha kwa njia ya
mdomo kusudio la kukata Rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ya kupinga
uamuzi wa dhamana uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana.

Novemba 15, mwaka huo, Mawakili wa Lema walipeleka maombi Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha wakiiomba Mahakama hiyo ipitie mwenendo na uamuzi
uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha uliozuia Lema asipewe
dhamana.

Novemba 17, Mawakili wa Serikali waliweka pingamizi za awali wakipinga Mahakama Kuu Kanda ya Arusha isisikilize maombi hayo.

Novemba 20, Mahakama hiyo ilikubali kusikiliza maombi hayo, ambayo
yalisikilizwa Novemba  22  na kukubali mbunge huyo kukata rufaa
kupinga uamuzi huo wa Mahakama ya chini.

Novemba 28, mawakili wa Serikali waliweka tena pingamizi wakiiomba
Mahakama hiyo isisikilize maombi ya rufaa juu ya dhamana ya Lema.

Desemba 2, mwaka jana Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilifuta Rufaa ya maombi ya
dhamana ya Lema, kwa sababu wakata rufaa waliikata nje ya muda.

Desemba 8, Mawakili wa Lema waliwasilisha maombi ya kuomba muda wa
kuwasilisha notisi ya nia ya kukata rufaa ya maombi ya dhamana ya
mbunge huyo.

Desemba 14, mwaka jana mabishano makali ya kisheria yaliibuka kati ya mawakili wa
pande zote ambapo mawakili wa  Jamhuri waliweka pingamizi mbili
wakiiomba mahakama hiyo isisikilize maombi hayo mbele ya Jaji Dk.
Modesta Opiyo.

Desemba 20, mwaka jana mahakama hiyo ilikubali maombi hayo ya kusikilizwa kwa
dhamana ya Lema.

Desemba 28, mwaka jana
Mahakama iliagiza pande zote mbili kuwasilisha hoja zao za rufaa kwa
njia ya maandishi ili mahakama hiyo itoe uamuzi Januari 4, mwaka huu.

Januari 4 mwaka huu, dhamana ya mbunge huyo iliendelea kuwa kitendawili
baada ya mawakili wa Serikali kukata Rufaa Mahakama ya Rufaa
Tanzania, kupinga Jaji Salma Maghimbi, kusikiliza rufaa yao wenyewe.

Februari 27 mwaka huu, Mahakama ya Rufaa Tanzania ilifuta rufaa mbili
za Jamhuri dhidi ya Lema baada ya Mawakili wa Serikali kuieleza
mahakama  hiyo kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), hana nia ya kuendelea na rufaa
hivyo kuiomba  kuzifuta rufaa hizo zilizokuwa zinahusu dhamana ya mbunge huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles