26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MADIWANI WAKOSA IMANI NA VIONGOZI WA SERIKALI

Na Upendo Mosha, Mwanga

BARAZA la madiwani wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, limesema halina imani na viongozi wote akiwamo Mkuu wa Wilaya hiyo, Aron Mbogho na vyombo vya ulinzi kutokana na kushindwa kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu vinavyoendelea katika Bwawa la Nyumba ya Mungu.

Pia baraza hilo la madiwani mwishoni mwa wiki iliyopita limeazimia kwa pamoja kumsimamisha kazi Ofisa Uvuvi wa Wilaya hiyo, Liberato Malisawa pamoja  na kuwaandikia barua kali za onyo maofisa wengine wadogo kadhaa wa uvuvi  kutokana na kushindwa kusimamia na kumaliza tatizo la uvuvi haramu linaloendelea kwa sasa katika bwawa hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho, baadhi ya madiwani hao ambao waliomba majina yao yasiandikwe gazetini, walisema kumekuwa na vitendo vya uvuvi haramu uliopitiliza unaoendelea kushamiri katika Bwawa la Nyumba ya Mungu, licha ya Serikali kupiga marufuku shughuli za uvuvi.

Walisema licha ya kuwapo vyombo vya ulinzi na usalama, bado vitendo hivyo vimeendelea kushamiri siku hadi siku na kwamba ofisa uvuvi wa wilaya hiyo hana sifa ya kuendelea kuwa mtumishi wa halmashauri hiyo kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Walisema kutokana na hali hiyo, madiwani wote kwa pamoja wameazimia kumsimamisha kazi  na kuwaandikia barua kali za onyo maofisa wengingine wadogo wa uvuvi kutokana na kushindwa kudhibiti uvuvi haramu.

Walisema mbali na hilo pia wamekosa imani na vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo Jeshi la Polisi pamoja na Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambaye ni Mkuu wa wilaya hiyo, Aron Mbogho.

Walisema samaki hao wamekuwa wakivushwa na kuuzwa huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiwapo, lakini hakuna hatua zozote za kisheria zinazochukuliwa kwa wahusika, jambo ambalo limesababisha madiwani kukosa imani na mwenyekiti wa kamati hiyo.

Akijibu tuhuma hizo wakati Akizungumza na MTANZANIA, Mbogho alikiri kupokea malalamiko hayo dhidi yake na kusema suala la vita ya uvuvi haramu ni la watu wote na si jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama tu wala ofisa uvuvi, bali linawahusu hata madiwani.

“Nimepata malalamiko japo si kiofisi, nafikiri nitayatapa rasmi kesho (leo), napenda kuwakumbusha madiwani kwamba bwawa  lile limezungukwa na wilaya tatu ambazo ni Simanjiro, Moshi Vijijini na Mwanga, suala la ulinzi ni jukumu la wilaya zote,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles