26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

UMASIKINI WA ROHO ZETU USITUGAWE WATANZANIA

Wananchi wakiwa kwenye mkutano
Wananchi wakiwa kwenye mkutano

NA TENGO KILUMANGA,

MARA nyingi  najiuliza hivi kuna ubaya  duniani? Kuna roho mbaya kweli? Na kama watu wapo wenye roho mbaya ni watu wa aina gani? Na ni sababu gani zinawafanya watu wengine kuwa na hisia  kama za namna hiyo? Ni kitu gani kinamfanya binadamu mwingine kumnyima au kumzibia mtu mwingine riziki yake?

Labda haya yote si kitu chenye ma​ajabu, ni tabia tu ya binadamu na hakuna kitu kibaya au kizuri, ila ni jinsi sisi binadamu  tunavyotaka kutafsiri mazingira yetu na kutokana na mahitaji hayo tunatengeneza mwongozo wa jinsi jumuiya itafanya kazi na kuheshimu mwitikio na matamanio ya wengi.

Woga ni miongoni mwa mambo ambayo mara nyingi unatufanya binadamu tunachukua uamuzi na kufanya vitendo ambavyo kikawaida viko chini ya utu na hadhi yetu. “Ukatili” ambao unakuja kwa sababu ya woga huo wa binaadamu  na mambo mengine ambayo yanasababishwa na vitendo kutokana na kutokuona mbali na kwa upana vinaturudisha nyuma sana kama jamii.

Nguvu nyingi unaweka kwenye kutengeneza mipaka kuliko kutafuta njia za kuimarisha mawasiliano kwa kupanga na kujenga mikakati na miundombinu chanya na maendeleo endelevu. Nguvu ya woga ni kubwa sana katika jamii  na jumuiya mbalimbali. Historia mara kwa mara imetuonesha madhara yake na ni kitu ambacho tujaribu sana tusikiruhusu kitufanye tupoteze imani kati yetu na kujenga hisia za kutokuelewana.

Ukishuka kwenye ngazii za watu utaona kwamba ubinafsi unaleta woga na watu wana ubinafsi sana utaona ni rahisi sana watu kama hao kuwa tayari kufanya mengi kuziba riziki ya mtu. Kujisikia woga ni kitu ambacho kinakuja kikawaida  ambacho binaadamu wote wanacho.

Kuna mstari mwembamba sana kati ya upendo na chuki, au hofu na imani. Hizi hisia zote zinafahamika na kusikiwa na watu mara kwa mara. Kitu gani kinaweza kukabiliana na hisia kama hizi na kuweza kupiga vita imani mbaya katika jamii? Kukabiliana na mawazo potofu hisia hii huleta katika jamii, ni misingi imara ambayo inaona kwa wote na kutendea haki wote.

Utamaduni mzuri, mazingira mazuri na mipango mizuri ambayo inatoa fursa kwa wote katika jamii. Katika jamii pia ni milango yote ipo wazi kwa yeyote ambaye anao uwezo wa kujenga maisha yake kwa mujibu wa sheria. Hapa ni Watanzania wote wanapewa nafasi hiyo, si wa ndani tu na wale wa nje pia.

Matumaini mapya na ndoto mpya juu ya kufanya mambo mapya, kiumbe kipya kinazaliwa na kuchukua mfumo mpya na kuja katika maisha. Moyo na roho ambazo zimejaa upendo wa kutaka kuendeleza katika kuwapo kwa mwongozo wa  kufanya mambo makubwa katika maisha yetu. kubeba mbegu za vizazi vyetu siku za nyuma mchanganyiko na mseto wa Mashariki-Magharibi na Afrika. Hii ni sababu ya sisi kuwapo duniani. Ni kwa ajili ya hiyo.

Dunia lazima iendelee na ukiangalia picha yote utaona sisi si lolote,  ni tone tu baharini lakini mambo binadamu wanayofanya ni makubwa kuliko binadamu wenyewe. Dhana shirikishi ambapo maisha hayana kizuizi na miili yetu ni vyombo na kiolesura nzuri kwa hata makuu zaidi, kifaa muhimu ambacho kimetubeba na kitaendelea kutubeba tu, enzi na enzi.

Vizazi vijavyo pengine vitaelewa kwamba kuna maisha katika kila kitu na vitu vyote na sisi ni kweli tumeungana na ni kitu kimoja, viumbe vilivyo hai au visivyo hai ni sisi sote ni yote yaliyotolewa mara kwa mara na bila kuchoka kutokana na uunganishi wetu na kuendelea kiroho na maisha ya nguvu.

Nami wakati wote nitakuwa mnyenyekevu na kushukuru mungu kwa ajili ya zawadi niliyopewa kwa mkopo kama baba na mzazi, kwa kuniwezesha kuwapa wanangu urithi wao kwa kule walikotoka na wao waweze kuwapa watoto wao, namshukuru Mungu kwa muda huu mfupi tuliopewa  wa kuendeleza tuliyoachiwa na vizazi vilivyopita na kuwapa vizazi vyetu tunayofahamu na thamani ya nafsi kugawana nao uzoefu wa maisha yetu na kuwasaidia wawe viumbe bora kuliko sisi milele.

Hiki ni kilio cha Wanadiaspora, tusinyimwe nafasi ya kuwapa watoto wetu chanzo cha shina lao, tusinyimwe pia kuwapa wenzetu tuliojifunza na tunayoyafahamu, kwani mwisho wa siku wote tumepata. Wanadiaspora wana mchango mkubwa sana na kwenye ngazi zote…​

Ukishafahamu haya yote, basi iliyobaki ni kasi tu ya kutekeleza uliyoyalenga..

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles