28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAMBO MUHIMU KWA WAPENZI WAPYA!

lovers

LEO nazungumzia juu ya mambo muhimu ambayo yanapaswa kuzingatiwa na wapenzi wanaoingia katika penzi jipya. Inawezekana ulikuwa unamsaka mwenzi wako kwa muda mrefu, lakini baada ya kumpata ukawa hujui mambo gani ya kufanya na yapi ya kuacha.

Ndiyo shabaha hasa ya mada hii. Kwamba kwa kuifuatilia kwa makini, utakuwa na mambo ya msingi yatakayokusaidia kwenye uhusiano wako.

Kama umeshampata mpenzi mpya, kitu kikubwa kinachotakiwa kuwa mbele ya fikra zako ni mambo gani muhimu ambayo unapaswa kumfanyia ili aweze kuamini kuwa unampenda.

MWAMBIE UNAMPENDA

Jambo la kwanza ambalo unapaswa kuzingatia ni kumhakikishia kwa mdomo na hisia kuwa unampenda, hata hivyo kumpenda huko kusiiishie kinywani pekee, bali hata matendo yako yanatakiwa yadhihirishe kile unachozungumza.

Ili aweze kuamini kuwa ni kweli unampenda kwa mapenzi ya kweli, kingine unachopaswa kufanya ni kuwa naye karibu kila wakati kwa njia ya mawasialiano.

Unapaswa kuwasiliana naye pale unapokuwa kazini au hata yeye anapokuwa katika shughuli zake. Ukifanya hivyo, ataamini kuwa unampenda ndiyo maana kila wakati unamkumbuka.

Unaweza ukampigia simu mchana ukamwambia: “Nakupenda sana mpenzi wangu, nashindwa kufanya kazi kutokana na kukumisi muda mrefu, angalau sasa nimeisikia sauti yako, naweza kufanya kazi kwa ufanisi.”

Ni maneno machache lakini yaliyobeba maana kubwa katika uhusiano wenu.

USIONGELEE FARAGHA

Baadhi ya marafiki huwa wana haraka ya kukimbilia kufanya ngono, acha nikuambie ukweli, kufanya ngono siyo mapenzi. Siku hizi hata wanawake wamekuwa wajanja sana, ukiwasumbua kuhusu kufanya tendo hilo mapema, wanajua kuwa huna mapenzi ya dhati kwao, hivyo wanakosa imani na wewe na kutoa nafasi ndogo ya kuendelea na uhusiano huo.

Usiwe na haraka rafiki yangu, kama kweli unampenda hutakiwi kuwa na haraka, subiri kwanza mpaka uhusiano wenu utakapokomaa ndiyo uanze kuzungumzia suala la mapenzi.

Katika hali ya kawaida, msichana anaweza akaamini kuwa ulimtamani ili ufanye naye mapenzi badala la kumwingiza katika mapenzi ya moja kwa moja yatakayowaingiza katika ndoa takatifu.

Usikubali mpenzi wako akawa na hisia mbaya na wewe mapema, ni vizuri zaidi kama utajitahidi kumfanyia mambo ambayo yatamfanya akuamini kuwa ni mkweli na mwenye mapenzi ya dhati kwake na huna lengo la kumchezea.

TOKENI PAMOJA

Siyo vibaya kama mtatenga siku moja kwa wiki kukutana na kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo katika penzi lenu ambalo kimsingi bado ni changa.

Toka naye ‘out’, kisha zungumza kwa furaha, mnaweza mkacheza michezo mbalimbali mkiwa ufukweni kama vile kukimbizana, kuogelea na mengine mingi, lakini kamwe msihusishe na mambo ya ngono mapema.

Kuanza uhusiano siyo kazi kubwa, kazi ni kuujenga uhusiano huo na kuwafanya kila mmoja wenu asiwe na raha pale asipomuona mwenza wake kwa wakati mmoja.

Lakini kazi nyingine kubwa ambayo itakuwa mbele yako ni jinsi ya kuweza kudumisha uhusiano huo kwa mpenzi wako na kuonesha nia yako ya dhati kwake kiasi cha kukufanya uweze kuvuka kuta za moyo wake na kuingia ndani zaidi.

Kiukweli kabisa, jambo hili linawashinda wengi na kujikuta wakiwapoteza wapenzi wao kwa kuwa huwa wanasumbuliwa na tamaa za haraka za kufurahisha miili yao badala ya mioyo ya wapenzi wao.

Usikose sehemu ya mwisho wiki ijayo.

Marafiki, kama unapenda kupata masomo haya zaidi kupitia ukurasa wetu wa WhatsApp wa Love Moment? Kama ndivyo tafadhali njoo inbox kwa namba zetu hapo juu, ukieleza ombi lako hilo, nasi tutakuunga ukutane na marafiki.

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano, ameandikia vitabu kama True Love, Let’s Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha SIRI ZA NDOA YENYE FURAHA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles