32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

AJABU LAKINI UKWELI KUHUSU MAPACHA

mapacha

JOSEPH HIZA NA MASHIRIKA YA HABARI,

MAPACHA ni watoto wawili wanaozaliwa kutoka mimba ile ile, ambao wamegawanyika katika aina mbili; wanaofanana na wale wasiofanana.

Karibu robo ya mapacha wote hufanana. Hii ina maana kwamba wametokana na yai moja lililotungwa na kujigawa katika makundi mawili tofauti ya chembechembe, kila moja hubadilika kuwa kiumbe pekee. Hadi sasa, wataalamu hawajafahamu vyema sababu za yai kujigawa.

Mapacha wa aina hii kwa vile wametokana na yai moja, mara nyingi huwa na jinsia moja na hufanana mno kimaumbile.

Mapacha wasiofanana hutokea wakati wa yai kupevuka, kokwa za mwanamke hutokea zikawa mayai mawili badala ya moja tu.

Mayai yote mawili hurutubishwa na hutungishwa mimba kwa mbegu mbili tofauti za mwanamume. Viumbe viwili hukua wakati mmoja katika mfuko wa uzazi. Mbali ya kukua katika mfuko mmoja wa uzazi na kuwa na umri uleule, mapacha hawa ni sawa sawa na watoto wengine wawili wa wazazi haohao. Wanaweza kuwa wa jinsia na maumbile tofauti kabisa.

Lakini tukiachana na hayo ambayo yanafahamika ijapokuwa ni sehemu ya maajabu ya uumbaji, kuna mengi ya kufurahisha, kushangaza na hata kuhuzunisha kuhusu mapacha ikiwamo baadhi kuzaliwa wakiwa wameungana kiasi cha kuhitaji operesheni kuwaokoa wote au angalau mmoja wao.

Kuna mengi kuhusu mapacha, ambayo huenda huyafahamu na miongoni mwao ni haya hapa chini;

Mapacha kuzaliwa kwa tofauti ya wiki hata miezi kadhaa

Katika kesi za nadra sana, hutokea kwa pacha mmoja kuzaliwa mapema kabla ya wakati, wakati mwenzake akiendelea kuwa ndani ya mimba kwa wiki na au hata miezi kadhaa. Katika kesi hii mapacha Amy & Katie wa Uingereza ni mfano halisi baada ya kuweka rekodi ya dunia kwa kuzaliwa tofauti ya siku 87 mwaka 2012. Amy Elliott alizaliwa mapema miezi minne kabla Juni Mosi 1, 2012 akiwa na uzito wa 1lb 3oz huku dada yake Katie akizaliwa Agosti 27. Ngumu kuamini? Ndiyo ukweli!.

Ajabu ya naoa za mapacha wafananao

Iwapo mapacha wa kiume wanaofanana wataoa mapacha wa kike wanaofanana, watoto wao si tu kwamba watakuwa binamu bali pia vinasaba vyao vitafanana kwa asilimia 50. Mara ngapi tukio kama hili hutokea? Si kawaida, lakini si jambo geni.

 Kitovu njia nzuri ya kutofautisha mapacha wafananao

Kuna wazazi hupata ugumu wa kutofautisha mapacha kiasi cha kuamua kuwapa alama. Lakini ipo njia nzuri;-kitovu.

Vitovu ni makovu na hivyo havina uhusiano wa kinasaba. Iwapo utatazama matumbo ya watoto utaona kwamba ijapokuwa baadhi ya vitovu vi sawa, na vitakuwa na tofauti. Ili kuwatofautisha, unachotakiwa ni kujiwekea kumbukumbu ya namna vitovu vyao vilivyo katika siku zao za mwanzo ili kuwatofautisha.

Shoto ni jambo la kawaida kwa mapacha.

 Moja ya mambo ya kufurahisha au kustaajabisha ni kwamba mapacha wengi ni wazuri kwa matumizi ya shoto iwe mikono au miguu.

 Mapacha kuzaliwa wanaume wawili tofauti

Iwapo mayai mawili yametolewa na tendo la ndoa kufanyika ndani ya vipindi vifupi toka wanaume wawili kabla au moja kwa moja baada ya uchavushaji wa yai, kuna uwezekano wa nusu kwa nusu wa watoto kuzaliwa na wanaume wawili tofauti.

Miongoni mwa kesi za aina hii, ni mama mkazi wa Texas nchini Marekani, Mia Washington ambaye alitembea nje ya ndoa na kujifungua watoto mapacha waliopishana dakika saba.

Yeye mwenyewe na madaktari wake waligundua mapacha hao Justin na Jordan Washington walizaliwa wakitokana na baba tofauti kwa vile hawafanani kabisa na mumewe. Mama alikiri kutembea nje ya ndoa yake na mumewe James Harrison.

 Mapacha kuwa wa utaifa tofauti

Ni ajabu lakini kweli. Iwapo mama wakati wa kipindi cha uchavushaji mayai yake mawili yanapatikana kwa mchakato huo na amefanya ngono na wanaume wawili tofauti wa rangi tofauti, anaweza kuzaa watoto si tu wa baba tofauti bali pia wa rangi tofauti. Licha ya utofauti wa rangi wanabakia bado mapacha.

Lakini pia kuna mapacha wanaozaliwa na rangi tofauti kutoka kwa baba yule yule iwapo wazazi ni wa rangi mchanganyiko. Hutokea mara moja kwa kila wenzi milioni moja wa vinasaba mseto. Imetokea katika kesi nadra. Kian na Renee ni mapacha lakini mmoja ana ngozi nyeupe na mwingine nyeusi na wote wa baba mmoja. Wow!

 Mapacha wanaweza kubuni lugha yao wenyewe

Utafiti uliofanywa na taasisi moja ya lugha nchini Marekani umeonesha kwamba watoto mapacha hujifunza matamshi baina yao wenyewe kwa njia ya kubwabwaja  na zaidi ya asilimia 40 huunda lugha tashtiti kwa mawasiliano baina yao wakingali wadogo. Lugha hiyo hakuna mwingine aijuayo zaidi yao tu.

 Mapacha huweza kuzaliwa na mapacha siku moja

Mapacha huweza kuzaa kwa siku moja na uwezekano ni kesi moja kati ya kesi milioni

 Mifumo tofauti ya kinga

Mapacha wafananao hawachangii mifumo inayofanana ya kinga mwilini ikimaanisha kwamba namna wanavyoitikia na hata kukabiliana na ugonjwa fulani kunaweza kuwa tofauti. Tafiti zilizowahi kufanyika zilionesha mapacha wa kiume wakipewa damu iliyoambukizwa virus. Mmoja alionekana kuwa na mfumo wenye afya wa kinga baada ya uambukizo huo wakati mwingine aliugua. Vitu vilivyo wazi ni kwamba mapacha wanapozaliwa kutoka tumboni huitikia tofauti katika kukabiliana na bakteria na virus wengineo, ikimaanisha kwamba mifumo yao ya kinga haifanani.

 Mapacha hurefusha urefu wa maisha ya mama zao

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utah, nchini Marekani miongo mingi iliyopita umeonesha kwamba watoto mapacha hurefusha maisha ya mama, yaani mama mwenye watoto mapacha ana uwezekano wa kuishi miaka mingi sana kuliko asiye na mapacha

 Hawafanani alama za vidole

Kila mtu duniani ana kinasaba chake ingawa ni tofauti kwa mapacha wa kulandana kwani vinasaba vyao viko sawa. Lakini hutofautiana alama za vidole, ambazo ingawa hulandana wakati wakiwa kwenye kijusi, alama hizo huachana baada tu ya kijusi kutengana

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles