27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

TEKNOLOJIA YA KUTUMIA SIMU BILA KUHITAJI LAINI, VOCHA

lifestylenews

NA FARAJA MASINDE,

AFRIKA ni nyumbani hivyo hatuna budi kusapoti vipaji vyetu pindi vinapotokea haijalishi ni nyanja ipi ya ubunifu lazima tuupe uzito unaostahili.

Ni wazi kuwa kuna mambo mengi ya ubunifu ambayo yamekuwa yakipatikana Afrika lakini leo tunaangazia ubunifu unaofanywa kwenye eneo la teknolojia kwani ndiyo dhima ya safu hii kukupa yote muhimu ya utandawazi.

Najua fika kuwa utakuwa umesikia kwenye mataifa yaliyoendelea juu ya watu ambao wamekuwa wakifanya ugunguzi wa vitu mbalimbali vya teknolojia na hata kutufikia Afrika japo huchukua muda kidogo.

Leo ni zamu yetu ambapo mbunifu mmoja kutoka nchini Namibia amefanikiwa kutengeneza teknolojia inayoruhusu watu kupiga simu bila kuhitaji laini, vocha popote pale ulipo duniani.

Ni Simon Petrus, anayesoma katika shule ya Abraham Iyambo Senior, amefanikiwa kutengeneza simu hiyo kwa kutumia raslimali mbalimbali ambazo amezipata kutoka kwa wazazi wake.

Teknolojia hiyo imetumia vifaa kutoka kwenye simu na seti ya televisheni kuunda kifaa hicho ambacho hupata nguvu kutoka kwenye mawimbi ya tv na redio kupiga simu bila kuhitaji laini yoyote, je nini cha zaidi hapa?.

Cha zaidi hapa ni kuwa mtumiaji wa simu hiyo anao uwezo wa kuangalia chaneli mbalimbali za tv kupitia simu yake hiyo na anaamini kuwa teknolojia hiyo ya kutumia simu bila kuhitaji laini na vocha huenda ikavunja rekodi ya Afrika na hata nje ya Afrika.

Ni faraja kuona kuwa aina ya mapinduzi ya teknolojia ambayo tumekuwa tukiyaota kila siku yameanza kufikiwa Afrika, hivyo kuimarika kwa teknolojia hii itakuwa ni jambo la kupongezwa na wapenda teknolojia.

Satellite hiyo iliyobuniwa na kijana huyo inaaminika kuwa imara zaidi hasa kwenye kuunganisha mtandao wa intaneti ambapo ukubwa wa satellite hiyo unaweza kuibeba hata kwenye begi dogo kama lile la Laptop ambapo pia inajumuhisha poti za USB ambazo unaweza kuunganisha na modem, simu, tabiti na kifaa kingine huku ikiwa na spidi kubwa.

Petrus anasema kuwa huduma hiyo mpya itaanza kusambaa kote Afrika siku za usoni mara baada ya kupata ufadhili zaidi.

Licha ya kubuni simu mwaka jana kijana huyo alifanikiwa kutengeneza mashine ya kutayarisha mbegu za mazao ubunifu ambao ulimpatia medali ya dhahabu ya taifa.

0653045474

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles