25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

KUPUUZWA MAELEKEZO YA CAG CHANZO CHA UFISADI

3f0e671e-bb9a-4214-8b41-ee64ec2f7b2c

Na JUDITH NYANGE-MWANZA

KUTOZINGATIWA kwa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kumetajwa kama chanzo cha kuendelea kuwapo mmomonyoko wa maadili kwa watendaji wenye dhamana kutofuata au kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utawala bora.

Hayo yamebainishwa jana na Katibu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Fabian Pokela, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba na kuhudhuriwa na viongozi kutoka taasisi na mashirika mbalimbali ya Serikali.

Pokela alisema kutokuzingatiwa kwa ushauri uliomo katika taarifa hizo za CAG, kumechangia kuendelea kuwapo kwa upungufu na kasoro zinazoendelea kubainishwa kila mwaka katika halmashauri mbalimbali.

“Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hazifanyiwi kazi ipasavyo na maofisa masuuli ili kuleta tija katika kuboresha na kuimarisha  uwajibikaji, hali hii inasababisha kutozingatia na kutekeleza ipasavyo mapendekezo na ushauri unaotolewa katika taarifa hiyo,” alisema Pokela.

Alisema pamoja na kwamba majukumu ya CAG ni kutoa mapendekezo na ushauri kwa kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa, lakini kumeendelea kuwapo kwa mmomonyoko wa maadili kwa watendaji wenye dhamana kwa kutofuata au kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utawala bora.

Pokela aliwataka wananchi kushiriki katika kuhimiza maadili katika ngazi zote kuanzia familia katika malezi ya watoto na vijana, hususani shuleni na hatimaye kuhimiza uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa katika ngazi zote za utumishi wa umma na uongozi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alisema Serikali ya awamu ya tano imeweka nguvu nyingi katika kuhakikisha  maadili ya viongozi wa umma yanazingatiwa ili kupambana na rushwa na vitendo vya ufisadi ambavyo vilikuwa vimekithiri katika jamii, hivyo ni vyema kila mtumishi akazingatia sheria kanuni na taratibu za utumishi wa umma katika utendaji wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles