27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

NCCR-Mageuzi yapuliza kipenga

mosenaJonas Mushi na Adamu Mkwepu, Dar es Salaam
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimetoa ratiba kwa wanachama wake kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Ratiba hiyo ilitangazwa jana na Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi, Mosena Nyambabe, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya chama hicho.
Alisema wanachama wenye sifa kwa mujibu wa katiba ya NCCR- Mageuzi pamoja na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wana haki ya kuwania nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge na urais.
“Kwa mujibu wa ratiba ya chama kuanzia Machi 15-30 mwaka huu, utakuwa ni muda wa kuchukua fomu kwa wanachama wenye sifa kwa mujibu wa katiba ya chama wanaotaka kuwania nafasi za uongozi kuanza kuchukua fomu na kwa upande wa wawakilishi na wabunge zoezi la kuchukua fomu litaanza Machi 20 na kumalizika Machi 31 mwaka huu,” alisema Nyambabe.
Alisema kwa wanachama wenye sifa za kuwania nafasi ya urais zoezi la kuchukua fomu litaanza Aprili mosi na kuhitimishwa Aprili 30 mwaka huu.
Nyabambe alisema bado chama hicho kinaendelea kukaribisha wanachama wapya na yeyote atakayejiunga nacho atakuwa na haki ya kuwania nafasi ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi.
“Endapo mtu atajiunga na chama chetu na akapewa kadi ya chama atakuwa na haki sawa na wanachama wengine na akijiunga kabla ya mchakato wa kuchukua fomu haujamalizika, atakuwa na haki ya kuchukua fomu na kuwania nafasi anayotaka,” alisema Nyambabe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles