27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yakiri matatizo ya waalimu kikwazo cha elimu

Patricia Kimelemeta

SERIKALI imekiri kuwa matatizo mbalimbali katika sekta ya elimu yanasababisha baadhi ya walimu kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo hali inayochangia kushasha elimu.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa ripoti ya hali ya elimu Tanzania iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Twaweza, Meneja Mawasiliano, Mipango na Usimamizi wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa

Dk. Shukuru Kawambwa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa

, alisema matatizo mbalimbali yanayowakabili walimu pamoja na serikali kuchelewa kuwalipa mishahara kwa wakati ni kikwazo kwa elimu.

Katika uzinduzi huo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam Rugaba alisema kitendo hicho kimesababisha baadhi ya walimu kutokuwa na moyo wa kufundisha, hali iliyosababisha baadhi yao kushindwa kutimiza majukumu.

“Sekta ya elimu ina changamoto nyingi ambazo zinatokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya walimu kutokuwa na moyo wa kufundisha.

“Hali hiyo inasababisha idadi kubwa ya wanafunzi kufeli na wengine kukosa masomo kutokana na walimu kutoingia madarasani,”alisema Rugaba.

Aliongeza kuwa mbali na matatizo hayo, pia kuna changamoto ya migogoro ya walimu inayotokana na ukosefu wa nyumba, madeni wanayoidai serikali na mishahara duni.

Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo, serikali ilianzisha mpango wa Matokeo Makubwa sasa(BRN) ili kuangalia matatizo hayo na kutafuta mbinu ya kuyatatua.

Hata hivyo Rugaba alisema baada ya kuona hivyo, serikali imejitahidi kulipa madeni ya walimu kwa zaidi ya asilimia 65 hali iliyosaidia kulipunguza deni hilo kwa kiasi kikubwa.

Katika kutatua matatizo ya walimu ili kuboresha elimu nchini, alisema serikali imepanga kujenga nyumba za walimu katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwa ni pamoja na kuwapa motisha wale watakaofanya vizuri kwenye shule zao ili kuwahamasisha wengine waweze kujituma zaidi.

Alisema walimu ambao shule zao hazitafanya vizuri kwenye mitihani, watawaita na kuzingumza nao ili waweze kujua tatizo lililopo na kulifanyia kazi.

Kwa upande wake mtafiti kutoka Twaweza, Constantine Manda alisema kuwa baada ya kufanya utafiti katika shule mbalimbali nchini walibaini kuwa asilimia 34 ya walimu ndio wanaoingia madarasani huku asilimia 38 hawaingii kabisa.

Alisema hali hiyo inamaanisha kuwa ni walimu watatu kati ya 10 ndio wanaoingia darasani katika muda wa vipindi.

Alisema tatizo hilo linasababishwa na waalimu kukosa moyo wa kufundisha, migogoro baina yao na serikali pamoja na hali ngumu za maisha.

Alisema kutokana na hali hiyo, serikali inapaswa kushughulikia matatizo hayo ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo yaliyopo hali itakayosaidia kupunguza ukubwa wa tatizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles