27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Donald Trump kumfukuza Arsene Wenger

arsene-wenger-donald-trump-quote-quotes-criticism-who-is-this-quiz-main-photoWASHINGTON, MAREKANI

RAIS mpya wa Marekani ambaye amechaguliwa jana, Donald Trump, aliwahi kusema kuwa akipata nafasi ya kuwa rais atamfukuza kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, kutokana na kushindwa kuipa klabu hiyo taji la Ligi Kuu nchini England kwa muda mrefu.

Rais huyo aliyasema hayo Machi mwaka huu mjini North Carolina, wakati wa kampeni zake za uchaguzi mkuu ambazo zilifikia tamati jana huko Marekani.

Trump alidai kuwa mashabiki wa klabu hiyo wamechoka na matokeo mabovu ambayo yanatokana na usajili wa wachezaji ambao hawana kiwango kikubwa, wakati huo mashabiki wanatamani kuiona timu yao ikitwaa mataji.

Inasemekana kuwa Trump ni shabiki namba moja wa klabu hiyo ya Arsenal, hivyo na yeye amekuwa miongoni mwa mashabiki ambao wamechoka kuiona timu yao ikikaa muda mrefu bila ya mataji.

Alisema kuwa umefika wakati wa kocha huyo kuondoka na kuwapisha wengine ambao watakuja na mifumo mipya na yakisasa kwa ajili ya maendeleo ya klabu hiyo.

“Mimi ni shabiki namba moja wa Arsenal FC na ni kweli mimi ni The Gunners, nilitarajia kuona tunazinyanyasa klabu nyingine, Arsene Wenger, anaziumiza nafsi nyingi za mashabiki wa Arsenal duniani nikiwa pamoja na mimi mwenyewe.

“Kocha huyo anaiendesha klabu hiyo kama yakwake binafsi hivyo hana wasi wasi na kile ambacho kinaendelea. Inakuwaje Manchester inatufunga? Si Man United tu hadi Swansea City, Wenger anakuwa kama keki bandia.

“Arsenal kwa sasa inaonekana ni klabu ya kujipigia na kila klabu. Inashangaza kuona klabu ya Man United na Chelsea ikitufunga nyumbani na ugenini.

“Wenger anaonekana kama mwigizaji wa filamu hakuna jipya ambalo atalifanya, kama klabu ina tatizo la fedha niko tayari kuzitoa kwa ajili ya kocha mpya ambaye atasajiliwa na nipo tayari kumpa kocha huyo mpya mshahara wa miaka 50.

“Ninachokitaka ni kuona Wenger akiondoka katika klabu hiyo kwa amani na kuiacha ikitafuta mafanikio mapya,” alisema Trump.

Hata hivyo, kocha huyo alitoa ushauri wa kuzitaka klabu za Manchester United pamoja na Chelsea kuungana pamoja na kuitengeneza timu kwa ajili ya kuifunga Arsenal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles