28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji asimulia hukumu iliyomtesa

 

Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Engera Kileo, akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa mahakama hiyo, wakati wa hafl a ya kumuaga iliyofanyika Mahakama Kuu, Dar es Salaam jana.
Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Engera Kileo, akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa mahakama hiyo, wakati wa hafl a ya kumuaga iliyofanyika Mahakama Kuu, Dar es Salaam jana.

JOHANES RESPICHIUS Na ELIAS SIMON (TUDARCO)-Dar es Salaam

JAJI mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Engera Kileo, amesimulia kesi ambayo hawezi kuisahau katika maisha yake katika utumishi wake wote.

Vilevile amewataka watoa haki kuhakikisha haki inatendeka kwa kuzingatia vipengele vya ufundi ambavyo vinaweza kusababisha  kuchelewesha haki kutopatikana kwa wakati.

Akizungumza katika hafla ya kuagwa baada ya kustaafu,   Dar es Salaam jana, alisema kesi ambayo hataisahau inahusu mirathi.

Jaji Kileo ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), alitoa ushuhuda huo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari kuhusu kesi ambayo hataweza kuisahau katika maisha yake baada ya kustaafu utumishi wa umma.

Alisema hukumu hiyo ilihusu kesi ya mirathi ya mtoto yatima aliyekuwa anaishi na virusi vya Ukimwi ambaye ndugu walikuwa wameuza mali za wazazi wake.

Alisema usiku wa kuamkia siku ya hukumu hakupata usingizi huku akisubiri kupambazuke   aweze kutoa haki kwa mtoto huyo.

“Nimewahi kuletewa kesi ya mirathi iliyokuwa ikimuhusu mtoto ambaye alifiwa na wazazi wake, sasa ndugu waliokuwa wamebaki walitaka kumnyang’anya mali iliyokuwa imeachwa kwa bibi yake.

“Mtoto na bibi yake walikuwa wanaishi Bukoba mkoani Kagera, mtoto huyo alipoanza kuugua walimuacha mtaani akitangatanga, akaja kusaidiwa na watu wengine wakati huo ndugu zake walikuwa wameshauza nyumba.

“Siku hiyo sikulala usingizi nikiwaza kupambazuke  nitoe haki kwa yule mtoto na nilihakikisha anapata haki kama alivyoachiwa na wazazi wake,”alisema Jaji Kileo.

Kuhusu umuhimu wa haki, Jaji huyo alitoa wito kwa wahusika kuzingatia vipengele vya ufundi   kuepuka makosa ya kumhukumu mtu asiyekuwa na hatia.

“Kama Baba wa Taifa Mwalimu  Nyerere alivyowahi kusema kwamba ni bora watu 99 wenye hatia kuachiliwa huru kuliko mtu mmoja asiyekuwa na hatia kuhukumiwa,” alisema.

Jaji Kileo anastaafu huku akikumbukwa kushiriki katika kutoa hukumu kadhaa ikiwamo ya Aprili 23, 2013 ambayo kwa kusaidiana na majaji wengine, walitupilia mbali maombi ya makada  watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutaka chombo hicho kufanya mapitio ya hukumu ya Mahakama ya Rufani iliyomrejeshea ubunge, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) na kuamuru walalamikaji kulipa gharama zote za kesi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles