28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 17, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa awataka vijana kutumia fursa uwekezaji wa TEHAMA

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana kutumia fursa ya uwekezaji unaofanya na Serikali katika sekta ya TEHAMA ili kukuza uchumi binafsi na Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2024 wakati akimwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA, linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya Maonesho kwenye Kongamano hilo, Majaliwa ameipongeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wanasimamia ukuaji wa Sekta ya TEHAMA.

Amesema mkakati wa Serikali ni kujenga kituo ambacho kitakuwa na nafasi ya vijana watanzania wabunifu kwenda kubuni kazi zao nakuingia katika mifumo kuona tafiti mbalimbali.

Kaulimbinu ya Kongamano hilo ni “Kutumia Uwezo wa Akili Mnemba na Robotiki kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles