25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 15, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimia 51 waliopewa ajira mgodi wa North Mara ni wakazi wa Tarime

Na Malima Lubasha, Mara

Meneja Mahusiano wa mgodi wa dhahabu Barrick North Mara, Francis Uhadi, amesema asilimia 51 ya ajira katika mgodi huo niwananchi wa Mkoa wa Mara ambao wanatoka Nyamongo na Tarime.

Uhadi amesema hayo Oktoba 11,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa na ziara ya siku moja katika mgodi huo kuona utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii wanayotekeleza wilayani Tarime.

Amesema pamoja na kutoa asilimia hiyo ya ajira wameajiri walinzi 560 kutoka maeneo ya jirani na mgodi huo ikiwa ni kuzingatia ajira kwa wazawa na kusisitiza kwamba kitengo chake cha mahusiano kimekuwa kinatetea haki na maslahi yao ya ajira.

Uhadi ametoa wito kwa vijana kuacha vitendo vya uvamizi wa mgodi na kupora mawe badala yake wajiunge na vikundi ili waweze kupata fedha za kilimo na ufugaji kuongeza kipato chao na taifa .

Awali Meneja Mkuu wa mgodi huo, Apolinari Lyambiko akizungumza na waandishi hao wa habari alisema kuwa kwa kuna ongezeko la ajira kwa watanzania kwa asilimia 31 tofauti na kipindi cha nyuma amba po kulikuwa ni asiliia 20 pekee.

Lyambiko amesema asilimia 98 ya waajiriwa katika mgodi huo ni watanzania ambao asilimia 51 wanatoka mkoa wa Mara, pia mgodi umekuwa ni mchangiaji mkubwa serikalini.

Amesema mgodi huo unatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya afya, elimu, maji na mingine ya kijamii ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi Kenyangi inayojengwa Kata ya Matongo, utunzaji wa mazingira kuhakikisha wanaongeza uelewa kuangalia maji ya sumu yasilete ma dhara kwa wananchi.

Aidha Lyambiko amesema wameanzisha kitengo cha kupambana na malaria kuhakikisha jamii inayozunguka mgodi haipati malaria ambapo mwaka 2024/2025 wametenga bajeti ya sh 9.0 bilioni kutekeleza miradi 101 katika vijiji 11 vinavyozunguka mgodi.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kenyangi Khadija Sangi ameshukuru kampuni hiyo ya Barrichk North Mara kwa kuwajengea shule mpya yenye madarasa 12 ambavyo vitapunguza adha ya msongama no na utoro kwa baadhi ya wanafunzi.

Mwalimu Khadija amesema miundo mbinu ya shule ya awali ilikuwa na changamoto nyingi kwa kutuje ngea hii mpya imekuwa ni kichocheo mahudhurio ya wanafunzi kuongezeka hivyo itafunguliwa mwezi Januari,2025 ambapo darasa la saba wapo 88 kwenye darasa moja watakapohamia shule mpya wataku wa wanafunzi 45.

Amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 816,walimu 9,vyoo matundu 24 wavulana kwa wasichana, kila darasa lina madawati, meza na viti, jengo la utawala, nyumba ya mwalimu mkuu na nyumba 3 za wali mu za 2:1 pia vipo viwanja mbalimbali vya michezo.

Mkazi wa Kitongoji cha Kegonga A Lameck Chacha ambaye ni Katibu wa kikundi cha kilimo biashara ame sema mradi huo wa bustani kilimo cha umwagiliaji mboga mboga ulianzishwa na mgodi na umemsaidia ambapo umemuwezesha kusomesha watoto wake watatu na kununua ng’ombe 2 wa maziwa na lishe kwa familia.

Hata hivyo mgodi huo unasimamia vikundi mbalimbali vya kilimo cha mboga mboga mafunzo ambayo yalianzishwa na mgodihuo kwa lengo la kuinua jamii kiuchumi ikiwa ni pamoja na njia bora ya kujiajiri kuliko kuamini kwamba ni lazima kuvamia mgodi kupata mabaki ya dhahabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles