29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi za huduma za afya zaonywa utupaji taka hovyo

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limetoa siku 90 kwa taasisi zinazotoa huduma ya afya nchini kuzingatia matakwa ya sheria za mazingira na kuacha kutupa taka hovyo.

Akizungumza leo Mei 16,2024 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa NEMC, Hamad Kissiwa amesema kuna ukiukwaji wa sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake juu ya usimamizi na utupwaji wa taka hatarishi zinazotokana na huduma za afya.

Ameeleza kuwa taka hatarishi ni madawa yaliyotumika , taka zenye mgando wa damu, sehemu za mwili wa binadamu zilizoondolewa sababu za magonjwa mbalimbali, taka zenye viambukizi vya magonjwa, vitu vyenye nchi kali na zinginezo

“Taasisi za huduma ya afya zinatakiwa kufuata sheria ya mazingira na kanuni zake pamoja na miongozo ya wizara ya afya, tunatoa tahadhari kwa yeyote anaeyejishughulisha na shughuli hizi kuacha mara moja utupaji taka ovyo na ndani ya siku 90 kuweza kujisajili kwenye wizara husika ili kupata utaratibu mzuri kupata vibali maalum vya usimamizi wa taka hizi,”amesema Kissiwa.

Amesema taka hizo ni hatarishi kwa afya ya binadamu, viumbe hai na mazingira kama hazitaratibiwa na kusimamiwa ipasavyo ili kuzuia na kudhibiti athari hizo.

“Kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na taarifa na kushuhudiwa ukusanyaji, usafirishaji na utupaji taka holela wa taka zitokanazo na huduma ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.

“Hivyi ni dhahiri kuwa kuna baadhi ya watoa huduma za afya wasio waaminifu ambao wanakiuka matakwa ya sheria ya usimamizi wa mazingira sura ya 191 na kanuni zake kwa kusafirisha na kutupa taka ovyo zitokanazo na huduma ya afya bila kufuata utaratibu uliowekwa na sheria na wizara ya afya,”ameongeza.

Aidha amesema Baraza limezielekeza mamlaka za udhibiti nchini zinazoshughulikia usimamizi wa taka zitokanazo na huduma ya afya kuhakikisha kwamba waatoa huduma hizo nchini kote wanafuata miongozo iliyowekwa na wizara pamoja na masharti na kanuni za udhibiti na usimamizi wa taka zao uliowekwa na sheria na wizara ya afya.

Kissiwa amesema wanatarajia kufanya ukaguzi kupitia kanda zao zote ili kubaini wanaoenda kinyume na sheria kuanzia vituo vya afya, zahanati na hospitali kuu huku wanaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu mazingira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles