Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Mwanariadha Felix Simbu atakuwa miongoni mwa washiriki wa mbio za maadhimisho ya Siku ya Afrika ‘Africa Day Marathon’, akiungana na mabalozi mbalimbali wa Afrika wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Mbio hizo zilizoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Umoja wa Mabalozi nchini (ADG), zinatarajia kufanyika Mei 18, 2024 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 15, 2024, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ali Bujiku amesema wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kumbia riadha kwa sababu ni moja ya mchezo mkubwa duniani.
Amesema mbio zitakuwa za kilomita 5 na 15 ambapo mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania watashiriki na kila mmoja atashiriki na wafanyakazi wake wa idara mbalimbali za balozi hizo.
“Haya ni maadhimisho ya miaka 61 ya Umoja wa Afrika ambayo kilele chake ni Mei 25. Pamoja na mbio za marathon kunakuwa na utoaji wa misaada katika shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum zilizopo Dar es Salaam,” amesema Balozi Bujiku.
Naye Balozi wa Morocco nchini Zakari El Goumiri ambaye atakimbia kilomita 15, amesema mbio hizo zinaimarisha umoja wao kama mabalozi na kutoa mchango wao kusapoti jitihada za Serikali ya Tanzania.
Kwa upande wake Balozi wa Kenya, Isaac Njenga, amesema riadha ni nzuri kwa kuwa itawafanya wenzao wengi kushiriki, kusudi likiwa kutoa mchango wao hasa katika elimu.
Akifafanua kuhusu mbio hizo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga, amesema mtu yoyote anaruhusiwa kuungana na mabalozi hao kushiriki mbio hizo ambapo anayehitaji anatakiwa kujisajili kwa kiasi cha fedha Sh. 30,000.
“Chochote kitakachopatikana katika mbio hizo, kitakwenda kwenye shule nne tulizozichagua ambazo ni Uhuru Mchanganyiko, Jeshi la Wokovu, Jangwani na P