29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yataja faida kuongezeka Majaji wa Rufani

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Mahakama ya Tanzania imetaja faida za kuongezeka kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kuwa ni pamoja na kupunguza mrundikano wa mashauri.

Faida zingine ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi katika Masjala zote za Mahakama Kuu, mashauri kusajiliwa na kuamuriwa kwa wakati na kupunguza mzigo kwa majopo yaliyokuwepo.

Hayo yameelezwa leo Aprili 5,2024 na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Prof Ole Gabriel amesema wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kumekuwepo na ongezeko la Majaji wa Rufani.

Amesema ongezeko la Majaji wa Mahakama ya Rufani limeenda sambamba na uanzishwaji wa Masjala ndogo ya hiyo nchini.

Amesema wakati Dk Samia Suluhu Hassan akiingia madarakani Machi 2021 kulikuwa na Majaji wa Rufani 16.

“Na katika uongozi wake hadi kufikia 03 Septemba 2023 idadi ya Majaji wa Rufani imeongezeka na kufikia 35 ikiwa ni zaidi asilimia 100. 

Amesema ongezeko la Majaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa linawezesha majopo 11 ya majaji watatu, majopo saba ya majaji watano na majopo matano ya majaji saba kuendesha vikao vya Mahakama ya Rufani kwa wakati mmoja.

Amesema idadi ya vituo vya kusikilizia mashauri ya Mahakama ya Rufani imeongezeka na kutoka 16 wakati wa Dk Samia akiingia madarakani na kufikia vituo 18 mpaka sasa. 

Amesema vituo vya usikilizaji wa mashauri ya Mahakama ya Rufani viko katika Masjala za Mahakama Kuu za Arusha, Dar es Salaam, Bukoba, Dodoma, Iringa, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Moshi, Musoma, Mtwara, Mwanza, Shinyanga, Songea, Sumbawanga, Tabora, Tanga na Zanzibar.

“Ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Pemba, ambao utaanza hivi karibuni ni miongoni mwa mafanikio yanayolenga kusongeza huduma za utopaji haki karibu na wananchi.

“Uwepo wa kituo hicho utaiwezesha Mahakama ya Rufani kuwa na Masjala yake ndogo, hivyo kuongeza idadi ya vikao vya mahakama kwa upande wa Zanzibar,”amesema Mtendaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles