25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Moto wateketeza vyumba 20 vya kulala wanafunzi

Wafanyakazi wa  Shule ya sekondari ya African Muslim iliyopo mjini Moshi,wakifanya jitihada za kuzima moto kwenye Bweni la wasichana wa shule hiyo uliosababishwa na hitilafu ya umeme  juzi usiku. Picha na Fadhili Athumani
Wafanyakazi wa Shule ya sekondari ya African Muslim iliyopo mjini Moshi,wakifanya jitihada za kuzima moto kwenye Bweni la wasichana wa shule hiyo uliosababishwa na hitilafu ya umeme juzi usiku. Picha na Fadhili Athumani

FADHILI ATHUMANI NA SAFINA SARWATT, MOSHI

VYUMBA 20 vya bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya African Muslim, iliyoko Kata ya Kaloleni, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, vimeteketea kwa moto.

Moto huo ambao ulizuka juzi saa 1:45 jioni na kuwaka kwa zaidi ya saa tano, ulianzia katika choo cha shule hiyo, jirani na Bweni la Makka kabla ya kuruka kwenye chumba cha jirani na kusambaa kwenye vyumba 20 vilivyoko katika bweni hilo.

Akizungumza na MTANZANIA katika eneo la tukio, Mkurugenzi wa Shule hiyo, Ali Adam Ali, alisema moto huo ambao hadi sasa chanzo chake hakijajulikana japo inadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme, umesababisha hasara kubwa kwa wanafunzi zaidi ya 96 wa kidato cha nne wanaotumia bweni hilo.

“Moto huu ulianza majira ya saa mbili kasoro, wanafunzi walikuwa wanajiandaa kuingia katika swala ya Isha, mmoja wa wanafunzi alihisi harufu ya moto na kuwajuza wenzie, baadae wakaanza kuhangaika kutafuta ni wapi chanzo chake kilipo, waligundua kuwa ulianzia chooni, ghafla ukasambaa katika vyumba vingine vya ghorofani kupitia chumba cha jirani na choo,” alisema Ali.

Alisema hakukuwa na madhara makubwa yaliyotokana na moto huo kutokana na wanafunzi wengi kuwa likizo, na kwamba ni wanafunzi wa kidato cha nne na kidato cha pili tu ndio walioathirika na moto huo.

“Hakuna majeraha makubwa kutokana na tahadhari ya kiusalama tuliyochukua kwa kushirikiana na uongozi wa Serikali ya Mtaa, wanafunzi walijitahidi kuondoa vitu vyao, vitanda na mabegi ya baadhi yao vimeungua katika moto, wanafunzi wanne walipoteza fahamu, tuliwakimbiza hospitali na sasa wanaendelea vizuri,” alisema Ali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Ibrahim Msengi, aliuagiza uongozi wa shule hiyo kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa na Ofisa Elimu wa mkoa kufanya tathimini ya hasara iliyotokana na moto huo.

Wakati huo huo, Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro, Estomih Makyara amemtaka mkurugenzi wa shule hiyo kutoa wiki moja ya mapumziko kwa wanafunzi walioathirika na moto huo, isipokuwa wanafunzi wa darasa la saba wanaoendelea na mitihani wataendelea kama kawaida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles