25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mradi JNHPP kivutio Zanzibar

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) umekuwa kivutio kwa wakazi  wa  Zanzibar kwa kuomba kupiga picha na bango la mradi huo wakati walipotembelea banda la Shirika la Umeme (Tanesco) katika  maonesho ya Kimataifa ya  biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya  Fumba.

Maonesho hayo yaliyoanza 7 Januari 7, 2024 ni  jitihada za Serikali katika uwekezaji wa Sekta ya nishati nchini.

Mmoja wa wadau waliotembelea banda hilo ni Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Selestine Kakele ambae ameonekana kuvutiwa na miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ikiwamo mradi JNHPP ambao umefikia asilimia 95.83.

Naye  Mwangulumba  kutola Bodi ya Taifa ya Pamba,  amesema kuwa mradi wa JNHPP ni tumaini jipya kwa Tanzania na kuwa utekelezaji wake umekua wa kipekee.

“Najiuliza tumewezaje kulifanya hili, huu mradi wa kipekee , maono ya waasisi wetu yalikua makubwa sasa hata wale  wanatuoshangaa, hili tumeliweza,”  amesema.

Kwa upande wake Issa Waziri mkazi wa Pemba, amesema kuwa mradi huo si kwamba utawapatia umeme wa kutosha lakini umekuwa kivutio kwa namna unavyoonekana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles