25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Afrika yatakiwa kuharakisha mazingira bora kwa wanawake kufanya biashara

Na Esther Mnyika,Mtanzania Digital 

Makamu wa kwanza wa Rais  wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema kuna  haja kwa Afrika kuharakisha uwekaji wa mazingira bora ya kuwezesha ushiriki thabiti wa wanawake katika  biashara ili kuweza kuzalisha  ajira nyingi nakufikia  maendeleo endelevu.

Akizungumza leo Desemba 8,2023 jijini Dar es Salaam katika hafla ya ufungaji wa  kongamano la pili la wanawake katika biashara ndani ya eneo huru la biashara barani Afrika, amesema nchi za Afrika zinapaswa kuchukua hatua ili kuwa na mabadiliko ya haraka ya kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika biashara. 

“Ni imani yangu kwamba katika siku tatu za majadiliano katika kongamano hili kila mmoja ameongeza uzoefu na uelewa wa namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo katika biashara ndani ya eneo Huru la biashara Barani Afrika”amesema.

Amesema ili kukabiliana na changamoto zilizobainishwa nchi zote za Afrika hazina budi kuwa na dhamira ya dhati ya kutekeleza maazimio yaliyofikiwa katika majadiliano .

Ameeleza kuwa kukiwa na nia thabiti ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa ,kutatoa hamasa kwa nchi rafiki na washirika wa maendeleo kwa kushirikiana na Bara la Afrika ili kufikia lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia ushiriki wao katika biashara ndani ya eneo huru la biashara barani Afrika.

“Ni matumaini yangu kwamba maazimio ya kongamano hili yatakuwa chachu ya kuandaa na kutekeleza ajenda ya Dk.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinara wa uhamasishaji wa ushiriki wa wanawake katika biashara ndani ya eneo huru la biashara barani Afrika”amesema.

Naye Waziri  wa Maendeleo  ya Jamii , Jinsia Wanawake  na Watoto  wa Zanzibar,  Riziki Pembe Juma  aliwahamasisha  wanawake wafanya biashara kuendelea kuongeza kasi ya uzalishaji wa bidhaa na utafutaji wa soko la bidhaa wanazozalisha ndani na nje ya bara la Afrika.

Kongamano  la pili la wanawake katika biashara ndani ya eneo huru la biashara barani Afrika limewakutanisha wadau wa sekta ya biashara  kutoka nchi 55 za bara la Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles