28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake kuwezeshwa kibiashara

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital 

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amesema serikali imejipanga kuwasaidia wanawake katika biashara ikiwemo kuwapa mitaji na teknolojia sahihi ya ufanyaji biashara na kuweka miundombinu wezeshi ili waweze kuingia kwenye soko huru la biashara barani Afrika.

Hayo ameyasema Desemba 7,2023 jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la wanawake eneo la  biashara huru Barani Afrika linaloendelea

kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) .

Amesema nchi imeendelea kuimarisha upatikanaji wa mitaji kupitia taasisi za fedha ikiwamo mabenki na taasisi nyingine lakini pia wizara kupitia SIDO wanatoa mafuzo ya ujasiliamali, mitaji kwa lengo la kumuwezesha mwanamke katika biashara.

“Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara kwa wanawake tu,lakini wizara kupitia Shirika letu la viwanda vidogo SIDO tunatoa mafunzo ya ujasiliamali, mitaji kwa mkopo lakini pia kuna fedha zinazokopeshwa kupitia halmashauri kwa ajili ya kuwasaidia wanawake vijana na makundi maalum,”amesema Kigahe.

Ameongeza kuwa fedha zinazotolewa na halmashauri zimeboreshwa ili kusaidia wajasiliamali kukuza biashara zao na kuwa kubwa ili ziweze kuingia kwenye ushindani wa masoko makubwa.

Amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wengine kama  SIDO wanasaidia wajasiliamali hao kupata teknolojia rahisi na sahihi ili kuzalisha kwa wingi bidhaa zao kwenye maeneo yao.

“Eneo la biashara Afrika lina nchi zaidi ya 55 ambazo zinaweza zikafanyabiashara ya pamoja, hivyo Tanzania inafursa hiyo kubwa ya kufanyabiashara kwani kuna bidhaa nyingi zinazozalishwa  kama mkonge,”amesema Kigahe.

Akizungumzia mkonge amesema ni moja ya bidhaa ambayo inahitajika sana kwenye soko la kimataifa hasa Afrika, kwani mkonge ukichakatwa inatumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo urembo na ujenzi.

“Mkonge unatumika katika ujenzi na unasaidia kupunguza joto, hii teknolojia ambayo tukiitumia hata sisi itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira lakini pia gharama za uendeshaji,”amesema 

Amesema serikali imeboresha miundombinu ya usafirishaji wa bidhaa,hivyo ametoa wito kwa wajasiliamali kushiriki ili kuchangamikia fursa lakini wanawaweke wajasiriamali kushirikiana na wengine kutoka nchi nyingine ili kubadilishana uzoefu na kutengeneza mtandao.

Naye Katibu Mkuu Mstaafu  wa Jumuiya ya Wanawake Nchi (UWT), Asma Mwilima amesema wanawake wafanyabiashara wanapata vikwazo mbalimbali pindi wanaposafirisha bidhaa zao nje ya nchi, hivyo kongamano hilo ni la muhimu kwani wanatumia jukwaa hilo kujadili changamoto zao na kuzifikisha kwa wahusika.

Kwa Upande wake Waziri  na  Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto  Zanzibar, Riziki Pembe Juma, ametoa rai kwa wanawake kujitokeza kwenye makongamano hayo kwani yanatoa fursa mbalimbali kwa wanawake hasa katika kujiendeleza kibiashara.

“Niwaombe sana wanawake wenzangu wa Bara na Zanzibar tutumie fursa ambayo marais wetu wametusogezea ili kuona wanawake tunafarijika na kuondokana na utegemezi wa kiuchumi na ukizingatia mwanamke sasa ameshakuwa Rais hivyo hatupaswi kurudi nyuma tunapaswa kwenda mbele,”amesema Juma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles